Swali: Je, anayeswali peke yake alipe Rak´ah nyinine au asujudu sijda ya kusahau endapo atakuwa na shaka kama amesoma al-Faatihah au hakusoma?

Jibu: Akitilia shaka mswaliji juu ya usomaji wa al-Faatihah ni kana kwamba hakuisoma. Akitilia shaka ya kuacha Rukuu´, Sujuud au kisomo [cha al-Faatihah] basi ni kana kwamba hakuifanya. Katika hali hiyo atatakiwa kuitekeleza. Isipokuwa akiwa ni mtu mwenye wasiwasi. Hivyo atatakiwa kutupilia mbali shaka hiyo. Ama akiwa ni mtu wa kawaida na si mwenye wasiwasi mara nyingi, akitilia shaka juu ya kuacha nguzo ni kama vile ameiacha na hivyo ni atatakiwa kuileta.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (20)
  • Imechapishwa: 08/06/2021