Wakati wa kutoa Zakaat-ul-Fitwr kwa mujibu wa Maalik

Nilimuuliza Ibn-ul-Qaasim wakati ambapo Maalik anapendekeza kutolewa kwa Zakaat-ul-Fitwr.  Akasema:

“Kabla ya kwenda katika uwanja wa kuswalia. Hata hivyo hapana vibaya kuitoa siku moja au mbili kabla.

Maalik amesema:

“Inapendekezwa kula kabla ya kwenda katika uwanja wa kuswalia siku ya Fitwr.”

Amesema:

“Maalik alinambia kwamba ameona wanazuoni wakipendekeza kutoa Zakaat-ul-Fitwr baada ya alfajiri ile siku ya Fitwr na kabla ya kuondoka katika uwanja wa kuswalia.”

Maalik amesema:

“Kuna wasaa katika jambo hili; ama mtu atoe kabla ya swalah au pia baada ya swalah.”

Maalik amesema:

“Naafiy’ alinambia kwamba Ibn Umar aliwaagizia Zakaat-ul-Fitwr wasambazaji siku mbili hadi tatu kabla ya siku ya Fitwr.”

  • Mhusika: Imaam Sahnuun bin Sa´iyd at-Tanuukhiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Mudawwanah al-Kubraa (1/110)
  • Imechapishwa: 28/04/2022