Zakaat-ul-Fitwr ya masikini kwa mujibu wa Maalik

Nilimuuliza Ibn-ul-Qaasim iwapo mtu anayestahiki kutoa Zakaat-ul-Fitwr pia anatakiwa kutoa Zakaat-ul-Fitwr kwa mujibu wa Maalik. Akajibu ndio.

Nilimuuliza kama wahitaji wanalazimika kutoa Zakaat-ul-Fitwr. Akajibu:

Maalik alinambia: “Kama anaweza kufanya hivyo, basi atafanya.”

Kisha tukamuuliza ikiwa anaweza kupata mtu awezaye kumkopesha pesa. Akajibu:

“Basi anaweza kukopa na kutoa.”

Nilimuuliza kuhusu wahitaji ambao hawawezi kukopa wala kuwa na uwezo wa kulipa Zakaat-ul-Fiwt kwa miaka yote iliyopita; ni lazima afanye hivo? Akasema:

“Hapana. Hayo ni maoni ya Maalik na maoni yangu.”

Maalik pia alisema:

“Yeyote anayechelewesha Zakaat-ul-Fitwr kwa miaka kadhaa basi ni lazima alipe kwa miaka yote iliyopita.”

  • Mhusika: Imaam Sahnuun bin Sa´iyd at-Tanuukhiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Mudawwanah al-Kubraa (1/109-110)
  • Imechapishwa: 28/04/2022