11. Ulazima wa kuingia katika Uislamu kikamilifu

Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

Allaah (Tabaarak wa Ta´ala) amesema:

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا ادْخُلُوا فِي السِّلْمِ كَافَّةً وَلَا تَتَّبِعُوا خُطُوَاتِ الشَّيْطَانِ ۚ إِنَّهُ لَكُمْ عَدُوٌّ مُّبِينٌ

“Enyi mlioamini! Jisalimisheni kikamilifu na wala msifuate hatua za Shaytwaan – hakika yeye kwenu ni adui wa wazi.” (02:208)

أَلَمْ تَرَ إِلَى الَّذِينَ يَزْعُمُونَ أَنَّهُمْ آمَنُواْ بِمَا أُنزِلَ إِلَيْكَ وَمَا أُنزِلَ مِن قَبْلِكَ يُرِيدُونَ أَن يَتَحَاكَمُواْ إِلَى الطَّاغُوتِ وَقَدْ أُمِرُواْ أَن يَكْفُرُواْ بِهِ وَيُرِيدُ الشَّيْطَانُ أَن يُضِلَّهُمْ ضَلاَلاً بَعِيدًا

”Je, huoni wale ambao wanadai kwamba wao wameamini yaliyoteremshwa kwako na yale yaliyoteremshwa kabla yako, wanataka wahukumiane kwa Twaaghuut na hali wameamrishwa wakanushe hiyo, na shaytwaan anataka awapoteze upotofu wa mbali kabisa.” (04:60)

إِنَّ الَّذِينَ فَرَّقُوا دِينَهُمْ وَكَانُوا شِيَعًا لَّسْتَ مِنْهُمْ فِي شَيْءٍ ۚ إِنَّمَا أَمْرُهُمْ إِلَى اللَّـهِ ثُمَّ يُنَبِّئُهُم بِمَا كَانُوا يَفْعَلُونَ

“Hakika wale waliofarikisha dini yao na wakawa makundi makundi huna lolote kuhusiana na wao. Hakika amri yao iko kwa Allaah, kisha atawajulisha kwa yale waliyokuwa wakifanya.” (06:159)

MAELEZO

Hili ndio jambo la lazima kuingia katika Uislamu kikamilifu na si baadhi yake:

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا ادْخُلُوا فِي السِّلْمِ كَافَّةً وَلَا تَتَّبِعُوا خُطُوَاتِ الشَّيْطَانِ ۚ إِنَّهُ لَكُمْ عَدُوٌّ مُّبِينٌ

“Enyi mlioamini! Jisalimisheni kikamilifu na wala msifuate hatua za Shaytwaan – hakika yeye kwenu ni adui wa wazi.”

Bi manaa ndani ya Uislamu.

إِنَّ الَّذِينَ فَرَّقُوا دِينَهُمْ وَكَانُوا شِيَعًا

“Hakika wale waliofarikisha dini yao na wakawa makundi makundi huna lolote kuhusiana na wao.”

إِنَّ الَّذِينَ يَكْفُرُونَ بِاللَّـهِ وَرُسُلِهِ وَيُرِيدُونَ أَن يُفَرِّقُوا بَيْنَ اللَّـهِ وَرُسُلِهِ وَيَقُولُونَ نُؤْمِنُ بِبَعْضٍ وَنَكْفُرُ بِبَعْضٍ وَيُرِيدُونَ أَن يَتَّخِذُوا بَيْنَ ذَٰلِكَ سَبِيلًا أُولَـٰئِكَ هُمُ الْكَافِرُونَ حَقًّا

“Hakika wale waliomkufuru Allaah na Mitume Wake na wanataka kufarikisha kati ya Allaah na Mitume Wake na wanasema: “Tunaamini baadhi [ya Mitume] na tunawakanusha wengine” na wanataka kuchukua njia iliyo baina ya hayo – hakika hao ndio makafiri wa kweli.” (04:150-151)

Kilicho cha lazima ni kuingia katika Uislamu kikamilifu. Kilicho cha lazima ni muislamu kushikamana na Uislamu kikamilifu inapokuja katika swalah, zakaah, swawm, hajj na jihaad. Kwa mfano haifai kwa mtu kusema kuwa ataswali lakini hatotoa zakaah, kwamba atatoa zakaah lakini hatofunga. Bali ni lazima kushikamana na Uislamu kikamilifu.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Fadhwl-il-Islaam, uk. 21
  • Imechapishwa: 19/10/2020