10. Baadhi ya mifano ya wito wa kipindi cha kikafiri

Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

Abul-´Abbaas amesema:

“Kila jina lenye kwenda kinyume na Uislamu na Qur-aan katika manasibisho ya ukoo, miji, makabila, madhehebu au mifumo ni katika sifa za kipindi cha kikafiri. Pindi mtu wa Muhaajiruun alipozozana na mtu wa Answaar na kila mmoja akawaita watu wake, ndipo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema:

“Mnaita wito wa kipindi cha kikafiri ilihali niko kati yenu?”

Akaghadhibika sana kutokana na hilo.”[1]

MAELEZO

Abul-´Abbaas ni Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah). Kinacholengwa ni kwamba kila wito usiohusiana na Uislamu, kama mfano wa ´enyi watu wa Makkah`, ´enyi watu wa Twaaif` na ´enyi watu wa Najd`, kunaingia katika katika wito wa kipindi cha kikafiri. Mtu aseme ´enyi waumini`, `enyi ndugu`, ´enyi Answaar` na ´enyi waja wa Allaah`.

Pindi mtu wa Muhaajiruun alipozozana.. – Uislamu ndio kitu cha lazima, ndio kinachokokoteza na kinachotikisa nyoyo zao. Wakati wanapokutana na adui kinachowapa nguvu ya kuwa imara na subira ni kuita kwa wito wa imani na Uislamu kama mfano wa kusema ´enyi waislamu`, ´enyi wanajeshi wa Allaah`, ´enyi waja wa Allaah`, ´enyi waislamu` na ´enyi wasaidizi wa Allaah`. Kinachowashaji´isha na kuwapa nguvu ni lile jina lililoenea.

[1] as-Siyaasah ash-Shar´iyyah (1/82).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Fadhwl-il-Islaam, uk. 19-20
  • Imechapishwa: 19/10/2020