Shari´ah ya Uislamu imekamilika kwa kila upande. Haina upungufu wala kasoro. Allaah (Ta´ala) amesema kuhusu uhakika huu uliothibiti:

الْيَوْمَ أَكْمَلْتُ لَكُمْ دِينَكُمْ وَأَتْمَمْتُ عَلَيْكُمْ نِعْمَتِي وَرَضِيتُ لَكُمُ الْإِسْلَامَ دِينًا

”Leo nimekukamilishieni dini yenu na nimekutimizieni neema Yangu na nimekuridhieni kwenu Uislamu uwe ndio dini yenu.”[1]

Hakuna chochote ambacho Ummahunakihitajia hivi sasa au huko baadaye, isipokuwa Allaah (Ta´ala) amekibainisha kwa njia ya kwamba Ummah kupitia kitu hicho umejua hukumu yake kama ni halali au ni haramu. Msingi huu umethibitishwa ndani ya Qur-aan na Sunnah na Ummah umeafikiana juu yake. Allaah (Ta´ala) amesema:

مَّا فَرَّطْنَا فِي الْكِتَابِ مِن شَيْءٍ

“Hatukupuuza katika Kitabu kitu chochote.”[2]

وَنَزَّلْنَا عَلَيْكَ الْكِتَابَ تِبْيَانًا لِّكُلِّ شَيْءٍ وَهُدًى وَرَحْمَةً وَبُشْرَىٰ لِلْمُسْلِمِينَ

“Tumekuteremshia Kitabu kikiwa ni chenye kuweka wazi kila kitu na ni mwongozo na rehema na bishara kwa waislamu.”[3]

وَكُلَّ شَيْءٍ فَصَّلْنَاهُ تَفْصِيلًا

”Na kila kitu Tumekipambanua waziwazi kabisa.”[4]

يَا أَهْلَ الْكِتَابِ قَدْ جَاءكُمْ رَسُولُنَا يُبَيِّنُ لَكُمْ كَثِيرًا مِّمَّا كُنتُمْ تُخْفُونَ مِنَ الْكِتَابِ وَيَعْفُو عَن كَثِيرٍ قَدْ جَاءكُم مِّنَ اللّهِ نُورٌ وَكِتَابٌ مُّبِينٌ يَهْدِي بِهِ اللّهُ مَنِ اتَّبَعَ رِضْوَانَهُ سُبُلَ السَّلاَمِ وَيُخْرِجُهُم مِّنِ الظُّلُمَاتِ إِلَى النُّورِ بِإِذْنِهِ وَيَهْدِيهِمْ إِلَى صِرَاطٍ مُّسْتَقِيمٍ

“Enyi watu wa Kitabu! Hakika amekujieni Mtume wetu ambaye anakubainishieni mengi katika yale mliyokuwa mkiyaficha katika Kitabu na anasamehe mengi. Hakika imekujieni kutoka kwa Allaah nuru na Kitabu kinachobainisha; Allaah kwacho anamwongoza yule atakayefuata radhi Zake katika njia za salama na anawatoa katika viza kuingia katika nuru kwa idhini Yake na anawaongoza katika njia iliyonyooka.”[5]

[1] 5:3

[2] 6:38

[3] 16:89

[4] 17:12

[5] 5:15-16

  • Mhusika: Shaykh ´Abdus-Salaam bin Barjas Aal ´Abdil-Kariym
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Hujaj al-Qawiyyah ´alaa anna Wasaa-il-ad-Da´wah Tawqiyfiyyah, uk. 16
  • Imechapishwa: 03/05/2023