Ambaye anakosa kumtakasia nia Allaah basi huyo ni mshirikina, na yule anayekosa ufuataji basi huyo ni mzushi. Ikishathibiti kuwa kulingania kwa Allaah ni ´ibaadah, basi mlinganizi anatakiwa kuzingatia sharti mbili hizi wakati wa kulingania kwake ili kitendo chake kiwe chema na chenye kukubaliwa. Ibn Qaasim (RahimahuAllaah) amesema:

“Ni lazima kulingania kwa Allaahkutimize sharti mbili:

1 –Ifanywe kwa ajili ya Allaah (Ta´ala) pekee.

2 – Kiafikiane na Sunnah za Mtume wa Allaah (SwallaAllaahu ´alayhi wa sallam).

Ikikosa sharti ya kwanza, basi anakuwa mshirikina, na ikikosa sharti ya pili, basi anakuwa mzushi.”[1]

Kutokana na hayo Salaf (RahimahumuAllaah) walikuwa ni wenye kupupia kutengeneza nia na matendo. ´Abdullaah bin Mas´uud (RahimahuAllaah) amesema:

“Sisi tunafuata na wala hatuzushi, tunaigiliza na wala hatuzui. Hatutopotea muda wa kuwa tumeshikamana na amri.”[2]

´Aliy na Ibn Mas´uud (RadhiyaAllaahu ´anhumaa) wote wawili wamesema:

“Maneno hayanufaishi isipokuwa kwa matendo, matendo hayanufaishi isipokuwa kwa maneno, maneno na matendo havinufaishi isipokuwa kwa nia, nai hainufaishi isipokuwa kwa kuafikiana na Sunnah.”[3]

Muhammad bin Siyriyn amesema:

“Walikuwa wakiona wako juu ya njia muda wa kuwa wamelazimiana na mapokezi.”[4]

Mutwarrif bin ´Abdillaah bin ash-Shukhayr amesema:

“Kutengemaa kwa moyo kunatokana na kutengemaa kwa matendo, kutengemaa kwa matendo kunatokana na kutengemaa kwa nia.”

Ibn ´Ajlaan amesema:

“Kitendo hakiwi sahihi isipokuwa kwa mambo matatu: kumcha Allaah, nia njema na kupatia.”[5]

Kuna mapokezi mengi kutoka kwa Salaf juu ya maudhui haya. Hapa ilikuwa ni kwa njia tu ya kuashiria.”

[1]Haashiyatu Kitaab-it-Tawhiyd, uk. 55

[2]Sharh Usuwl I´tiqaad Ahl-is-Sunnah wal-Jamaa´ah (1/86).

[3] ash-Shariy´ah, uk. 131, ya al-Aajurriy.

[4]Hilyat-ul-Awliyaa’ (2/199) ya Abu Nu´aym.

[5]al-Ikhlaasw wan-Niyyah ya Ibn Abiyd-Dunyaakupitia katika Jaamiy´-ul-´Uluum wal-Hikam (1/71) ya Ibn Rajab.

  • Mhusika: Shaykh ´Abdus-Salaam bin Barjas Aal ´Abdil-Kariym
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Hujaj al-Qawiyyah ´alaa anna Wasaa-il-ad-Da´wah Tawqiyfiyyah, uk. 14-15
  • Imechapishwa: 03/05/2023