Swali: Maimamu wengi wanapupia kukhitimisha Qur-aan katika Tarawiyh na Tahajjud ili kuwasikilizisha waswaliji Qur-aan yote. Je, kuna ubaya katika kufanya hivo?
Jibu: Hichi ni kitendo kizuri. Imamu kila usiku asome juzu au chini ya hapo. Lakini azidishe katika kumi la mwisho ili akhitimishe na kukamilisha Qur-aan. Hapa ni pale ambapo itakuwa ni wepesi pasi na uzito. Vivyo hivyo du´aa ya kukhitimisha Qur-aan imefanywa na wengi katika Salaf. Imethibiti ya kwamba Anas (Radhiya Allaahu ´anh) – ambaye alikuwa mfanya kazi wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) – kuwa alifanya hivo. Kuna kheri nyingi katika jambo hilo. Kilichowekwa katika Shari´ah ni waswaliji kuitikia du´aa ya imamu hali ya kutaraji Allaah atawakubalia. ´Allaamah Ibn-ul-Qayyim (Rahimahu Allaah) ameweka mlango katika kitabu chake “Jalaal-ul-Afhaam” ambapo humo ametaja hali za Salaf katika kupatiliza kukhitimisha Qur-aan. Napendekeza kukirejea ili kupata faida zaidi.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Fataawaa Swalaat-it-Taraawiyh, uk. 15
- Imechapishwa: 10/04/2022
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket