Ibn ´Uthaymiyn kuhusu kumuua kafiri anayesadizana na makafiri kuwapiga vita waislamu

Swali: Je, inajuzu kumuua kafiri akitamka shahaadah kabla ya vita kuanza?

Jibu: Haijuzu.

Muulizaji: Je, inajuzu kumuua vita ikianza kisha akatamka shahaadah?

Ibn ´Uthaymiyn: Akitamka shahaadah haijuzu kumuua.

Muulizaji: Vita imeshaanza?

Ibn ´Uthaymiyn: Sawa vita ikiwa imeshaanza au haijaanza. Kwa kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimkataza Usaamah bin Zayd alipomuua mshirikina baada ya yeye kusema laa ilaaha illa Allaah. Akawa anakariri kumwambia Usaamah:

“Je, umemuua baada ya yeye kusema laa ilalaha illa Allaah?”

Akasema alisema hivyo kwa ajili ya uoga. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akamkatalia na kumwambia. Usaamah akasema nilitamani nisingelikuwa muislamu. Lakini atamka shahaadah na kubaki katika safu za makafiri, muue. Lakini akisema hivi na kutoka katika safu zao, hii ni dalili ya ukweli wake. Akibaki ikiwa ni muislamu, atakuwa amewasaidia makafiri dhidi ya Waislamu. Hivyo kwa waislamu itakuwa ni halali kumuua. Atalipwa kwa nia yake na mbele ya Allaah. Hata akiwa ni mshirikina akatamka kwa ulimi wake, anastahiki kuuawa.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Liqaa’ al-Baab al-Maftuuh (166 B)
  • Imechapishwa: 10/04/2022