10. Bora kwa imamu ni yeye kukamilisha kisomo cha Qur-aan katika swalah ya Tarawiyh?

Swali: Bora kwa imamu ni yeye kukamilisha kisomo cha Qur-aan katika swalah ya Tarawiyh?

Jibu: Wigo ni mpana katika jambo hili. Sitambui dalili inayofahamisha kwamba bora ni kukamilisha kisomo. Isipokuwa baadhi ya wanazuoni wanaona kuwa inapendekeza kuwasikilizisha Qur-aan yote ili mkusanyiko upate kusikiliza Qur-aan yote. Hata hivyo hii sio dalili ya wazi. Jambo muhimu ni yeye kunyenyekea katika kisomo chake, apate utulivu, asome kwa utaratibu ipasavyo na awafaidishe watu ijapokuwa hatosoma isipokuwa nusu au theluthi ya Qur-aan. Muhimu sio yeye kukhitimisha. Muhimu ni yeye kuwanufaisha watu katika swalah yake, unyenyekevu wake na katika kisomo chake ili anufaike na apate utulivu. Ikimuwepesikia kukamilisha kisomo basi himdi zote anastahiki Allaah. Isipowepesika basi yanamtosha yale aliyoyafanya ingawa kutabaki baadhi ya sehemu. Kwa sababu kule kuwajali kwake watu, kupupia juu ya unyenyekevu wao na juu ya kuwafaidisha ni muhimu zaidi kuliko kukimbilia kukhitimisha. Akiwakamilishia bila uzito na akawasikilizisha Qur-aan yote ni jambo zuri.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Swalaat-it-Taraawiyh, uk. 13
  • Imechapishwa: 10/04/2022