Kitu kinachoshuhudia maneno yake kwamba sauti za kengele za mnara zinachukiza kwa hali zote, ni maneno yake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

”Kengele ni filimbi ya shaytwaan.”[1]

Imekuja katika upokezi mwingine:

”Malaika hawaandamani na matangamano yaliyo na kengele.”[2]

al-Munaawiy amesema:

”Kwa mujibu wa Ibn Hajar kinachochukiza ni ile sauti yake kwa sababu inafanana na kengele ya mnara na mfano wake.”

Hivi sasa kuna kengele mbalimbali zilizotengenezwa kwa malengo tofauti tofauti yenye manufaa, ikiwa ni pamoja na kengele ya kuamsha kutoka usingizini, kengele ya simu, kengele ya idara ya serikali na mfano wake. Je, hizi zinaingia ndani ya Hadiyth zinazokataza? Hapana, sionelei hivo. Kwa sababu hazifanani na kengele za mnara, si katika sauti wala muonekano wake – na Allaah ndiye mjuzi zaidi.

[1] Muslim, Abu Daawuud, al-Haakim, al-Khatwiyb al-Baghdaadiy, al-Bayhaqiy na Ahmad.

[2] Muslim kupitia kwa Abu Hurayrah na Abu Daawuud kupitia kwa Abu Salamah.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Jilbaab-ul-Mar-ah al-Muslimah, uk. 168-169
  • Imechapishwa: 01/11/2023