107 – Qataadah amesema:

”Wana wa israaiyl walikuwa wakisema: ”Ee Mola! Wewe uko juu ya mbingu na sisi tuko ardhini. Ni vipi tutajua radhi Zako kutokana na dhahabu Zako?” Akasema: ”Ninapokuwa radhi nanyi basi hukutawalishieni wabora wenu, na ninapokuwa nimewakasirikieni huwatawalishieni waovu wenu.”[1]

Haya yamethibiti kutoka kwa Qataadah, mmoja katika wanazuoni wakubwa wenye kuhifadhi.

108 – Saalim bin Abiyl-Ja´d amesema kuhusu maneno Yake (Ta´ala):

إِنَّ رَبَّكَ لَبِالْمِرْصَادِ

”Hakika Mola wako hapana shaka yoyote yutayari anaziona nyenendo zao zote!”[2]

”Upande mwingine wa Njia kuna madaraja. Kwenye daraja moja kuna amana. Kwenye daraja nyingine kuna kizazi. Kwenye daraja nyingine yuko Mola (´Azza wa Jall).”

Ameipokea al-´Assaal kwa cheni ya wapokezi Swahiyh[3].

109 – Maalik bin Diynaar amesema:

”Chukua na usome. Sikiliza maneno ya Mkweli kutoka juu ya ´Arshi Yake.”[4]

Ameipokea katika ”Hilyat-ul-Awliyaa” kwa cheni ya wapokezi Swahiyh[5].

[1] Ameipokea ad-Daarimiy katika hivyo vitabu viwili vilivyoashiriwa punde kwa cheni ya wapokezi nzuri.

[2] 89:14

[3] al-Bayhaqiy ameipokea katika ”al-Asmaa´ was-Swifaat”, uk. 432 kwa cheni ya wapokezi pungufu kupitia kwa Abu Fizaarah, kutoka kwa Saalim bin Abiyl-Ja´d. Abu Fizaarah alikuwa madhubuti na alikuwa akiitwa Raashid bin Kaysaan. Kisha baadaye al-Bayhaqiy akaipokea kwa cheni ya wapokezi yenye kuungana kupitia mwalimu wake al-Haakim (2/523), kutoka kwa al-A´mash, kutoka kwa Saalim bin Abiyl-Ja´d, kutoka kwa ´Abdullaah, na akasema:

”Haya ni maneno ya ´Abdullaah. Imesemekana kuwa ni Ibn Mas´uud (Radhiya Allaahu ´anh). Kwa maana hiyo ni kwamba kunakosekana kiunganishi baina yake yeye na Saalim bin Abiyl-Ja´d.”

Ni dhaifu kutoka kwa ´Abdullaah bin Mas´uud na ni Swahiyh kutoka kwa Saalim. Jukumu liko kwa mtunzi (Rahimahu Allaah), kwa sababu hakuonyesha cheni yake ya wapokezi ili tutoe maoni yetu juu yake. Kuhusu al-Haakim, ameisahihisha cheni ya wapokezi na adh-Dhahabiy akaafikiana naye.

[4] Hilyat-ul-Awliyaa’ (2/358).

[5] Hivo ndivo alivosema na Ibn-ul-Qayyim akaafikiana naye, uk. 105. Hata hivyo ni jambo linahitaji kuangaliwa vyema. Kwa sababu katika ”Hilyat-ul-Awliyaa” imesimuliwa kupitia njia mbili kutoka kwa Sayyaar: Ja´far ametuhadithia: Nimemsikia Maalik bin Diynaar.

Sayyaar bin Sulaymaan adh-Dhwuba´iy amesimulia kutoka kwa Ja´far bin Haatim al-´Anziy Abu Salamah al-Baswriy. Yeye ni kama alivosema Haafidhw katika ”Taqriyb-ud-Tahdhiyb”:

”Ni mkweli mwenye kukosea.”

adh-Dhahabiy amemtaja katika ”Mizaan-ul-I´tidaal” na akasema:

”Masimulizi yake yamesalimika. Ibn Hibbaan ameonelea kuwa ni mwenye kuaminika. ´Ubayd al-Qawaariyriy amesema:

”Hakuwa na uelewa. Tulikuwa pamoja dukani.” al-Qawaariyriy akaulizwa: ”Je, unamtuhumu?” Akasema: ”Hapana.”

al-Haakim amesema:

”Sayyaar alikuwa ni mfanya ´ibaadah zaidi katika zama zake. Ahmad bin Hanbal amesimulia sana kutoka kwake.”

al-Azdiy amesema:

”Amesimulia masimulizi dhaifu na yanayopingana.”

Imekuja tena katika ”at-Tahdhiyb”:

”Abu Ahmad al-Haakim amesema kwamba ”katika masimulizi yake kuna baadhi ya masimulizi dhaifu na yanayopingana.” al-´Uqayliy amesema kwamba ”masimulizi yake ni dhaifu na yanayopingana”. Ibn-ul-Madiyniy amemdhoofisha.”

Mfano wa mtu huyu cheni yake ya wapokezi haiwezi kuwa Swahiyh. Pengine hata haiwezi kusamehewa kule kusema kuwa ni nzuri. Haina neno kusimulia kutoka kwake – Allaah akitaka – muda wa kuwa hasimulii Hadiyth zenye kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) – na Allaah ndiye mjuzi zaidi.

  • Mhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-´Uluww lil-´Aliy al-Ghaffaar, uk. 126-128
  • Imechapishwa: 12/07/2024
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy