Ameendesha gari kwenye taa nyekundu na akaua mtembeaji kwa miguu

Swali: Kuna mtu ameendesha kwenye taa nyekundu makusudi na kuwaua watembea kwa miguu kwa bahati mbaya. Je, anazingatiwa kuwa ameua kwa makusudi?

Jibu: Wataamua mahakama. Uhalifu huo upelekwe mahakamani. Hata hivyo ni haramu kuwaweka wengine khatarini. Kuhusu fidia na mengine yapelekwe mahakamani.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (44)
  • Imechapishwa: 12/07/2024