104. Wanaume kujipamba kwa nguo nzuri kabisa siku ya ´iyd

Ni Sunnah kwa wanaume kujipamba na kuvaa mavazi yake mazuri kabisa. al-Bukhaariy amepokea katika “as-Swahiyh” yake kupitia kwa ´Abdullaah bin ´Umar (Radhiya Allaahu ´anhumaa) aliyesimulia:

“´Umar alichukua hariri nyororo – ambayo ilikuwa inauzwa sokoni – akaja nayo kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kusema: “Ee Mtume wa Allaah! Zinunue hizi na ujipambe nazo kwa ajili ya ´iyd na wajumbe.” Ndipo Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema:  “Hakika si vyengine ni kwamba haya ni mavazi ya wale wasiokuwa na fungu lolote.”

Alisema hivo kwa sababu ilikuwa hariri. Haijuzu kwa mwanaume kuvaa kitu katika hariri au katika dhahabu, kwa sababu ni haramu kwa wanaume wa ummah wa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

Kuhusu wanawake watoke kwenda kuswali ´iyd pasi na kujipamba, kujitia manukato, kuonyesha mapambo wala kuonyesha uso. Mwanamke ameamrishwa kujisitiri na amekatazwa kuonyesha mapambo na kujitia manukato wakati wa kutoka.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majaalis Shahr Ramadhwaan, uk. 225
  • Imechapishwa: 30/03/2024