Anayeamka mwishoni mwa wakati wa swalah – anaanza na faradhi au Sunnah?

Swali: Anayeamka mwishoni mwa wakati aanze kuswali swalah ya faradhi?

Jibu: Hapana, ataswali Raatibah kisha ndio aswali faradhi:

“Yule mwenye kupitikiwa na usingizi au akaisahau swalah, basi aiswali pale atapoikumbuka. Haina kafara nyingine isipokuwa hiyo.”[1]

Huu ndio wakati wake.

Swali: Hu ndio wakati wake lakini ataiswali kwa njia ya kuilipa?

Jibu: Kuna usahali katika jambo hilo. Ni mamoja ataita kuwa ni kuilipa au kuitekeleza. Jambo ni lenye usahali. Haidhuru.

[1] al-Bukhaariy (597) na Muslim (684).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23685/هل-يبدا-بالفريضة-ام-الراتبة-في-اخر-الوقت
  • Imechapishwa: 30/03/2024