Rawaatib na swalah za kujitolea zinakidhiwa?

Swali: Swalah zinazopendeza hazilipwi kabisa?

Jibu: Sunnah ya Dhuhr haikidhiwi baada ya ´Aswr.

Swali: Swalah zinazopendeza nyinginezo?

Jibu: Zinakidhiwa ndani ya wakati wake. Sunnah ya Dhuhr ya kabla inalipwa baada yake. Sunnah ya Fajr inalipwa baada yake. Sunnah ya ´Ishaa inakidhiwa usiku mzima. Hata hivyo bora zaidi ni kuikidhi kabla ya nusu ya usiku.

Swali: Anayeswali ´Aswr na hivyo akakumbuka kuwa hakuswali Sunnah ya Fajr?

Jibu: Ni Sunnah ambayo umepita wakati wake uliowekwa.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23684/حكم-ووقت-قضاء-النوافل-والسنن-الرواتب
  • Imechapishwa: 30/03/2024