104. Usijifananishe katika kuzungumza kwao

Allaah (Ta´ala) amesema:

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَقُولُوا رَاعِنَا وَقُولُوا انظُرْنَا وَاسْمَعُوا ۗ وَلِلْكَافِرِينَ عَذَابٌ أَلِيمٌ

”Enyi walioamini! Msiseme: ”Tusikilize!” lakini semeni: ”Tuangalie” –  na utusikilize; makafiri watapata adhabu iumizayo.”[1]

Haafidhw Ibn Kathiyr (Rahimahu Allaah) amesema:

”Allaah (Ta´ala) amewakataza waja Wake waumini kujifananisha na makafiri katika maneno na matendo yao. Mayahudi walikuwa wakitumia madokezo kwa lengo la kuwadhalilisha.

مِّنَ الَّذِينَ هَادُوا يُحَرِّفُونَ الْكَلِمَ عَن مَّوَاضِعِهِ وَيَقُولُونَ سَمِعْنَا وَعَصَيْنَا وَاسْمَعْ غَيْرَ مُسْمَعٍ وَرَاعِنَا لَيًّا بِأَلْسِنَتِهِمْ وَطَعْنًا فِي الدِّينِ ۚ وَلَوْ أَنَّهُمْ قَالُوا سَمِعْنَا وَأَطَعْنَا وَاسْمَعْ وَانظُرْنَا لَكَانَ خَيْرًا لَّهُمْ وَأَقْوَمَ وَلَـٰكِن لَّعَنَهُمُ اللَّـهُ بِكُفْرِهِمْ فَلَا يُؤْمِنُونَ إِلَّا قَلِيلًا

”Katika mayahudi wako wanayapotosha maneno kuyatoa mahali pake stahiki, na husema ”Tumesikia na tumeasi” na ”sikia bila ya kusikilizwa!” na ”Tusikilize!” – kwa kuzipotoa ndimi zao na kutukana dini. Na lau wangesema ”Tumesikia na tumetii” na ”Sikia na utuangalie”,  basi ingelikuwa kheri kwao na sawa zaidi. Lakini Allaah amewalaani kwa kufuru yao; basi hawaamini isipokuwa wachache tu.”[2]

Vivyo hivyo Hadiyth zimekuja kwamba pindi walipokuwa wanataka kutoa salamu walikuwa wakisema:

السام عليكم

”Kifo kiwe juu yenu.”

Wakimaanisha kifo. Kwa ajili hiyo tukaamrishwa kuwaitikia kwa kusema:

و عليكم

”Nanyi pia.”

Du´aa yetu dhidi yao inaitikiwa na si ya kwao dhidi yetu. Lengo hapa ni kwamba Allaah amewakataza waumini kujifananisha na makafiri katika maneno na matendo yao.”[3]

Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah) amesema wakati wa Aayah hii:

”Kwa mujibu wa Qataadah na wengineo mayahudi walikuwa wakisema hivo kwa ajili ya kuchezea shere; ndipo Allaah akachukizwa waumini kusema kama wanavosema wao. Amesema tena [Qataadah] kwamba mayahudi walikuwa wakimwambia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam): ”Tutegee sikio lako!”Wakisema hivo kwa njia ya kejeli. Neno hilo kwa mayahudi lilikuwa baya, jambo ambalo linajulisha kuwa waislamu wamekatazwa kulitamka, kwa sababu mosi mayahudi walikuwa wakilitamka, pili mayahudi walikuwa wanaliona vibaya. Ingawa neno hilo halikuwa baya kwa waislamu, wakakatazwa kutamka namna hiyo kutokana na kule kujifananisha na makafiri na mbinu zao wanazotumia kufikia malengo yao.”[4]

[1] 02:104

[2] 04:16

[3] Tafsiyr al-Qur-aan al-´Adhwiym (1/148).

[4] Iqtidhwaa’-us-Swiraat al-Mustaqiym, uk. 22

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Jilbaab-ul-Mar-ah al-Muslimah, uk. 164-165
  • Imechapishwa: 29/10/2023