103. Ususuwavu wa moyo sababu yake ni madhambi

Allaah (Tabaarak wa Ta´ala) amesema:

أَلَمْ يَأْنِ لِلَّذِينَ آمَنُوا أَن تَخْشَعَ قُلُوبُهُمْ لِذِكْرِ اللَّـهِ وَمَا نَزَلَ مِنَ الْحَقِّ وَلَا يَكُونُوا كَالَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ مِن قَبْلُ فَطَالَ عَلَيْهِمُ الْأَمَدُ فَقَسَتْ قُلُوبُهُمْ ۖ وَكَثِيرٌ مِّنْهُمْ فَاسِقُونَ

“Je, haujafika wakati kwa walioamini zinyenyekee nyoyo zao kwa ukumbusho wa Allaah na yale yaliyoteremka ya haki, na wala wasiwe kama wale waliopewa Kitabu kabla, ukawarefukia muda, halafu zikawa ngumu nyoyo zao – na wengi miongoni mwao wakatumbukia katika madhambi na kuasi?”[1]

Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah) amesema:

”Hapa kuna katazo kabisa la kujifananisha nao, khaswakhaswa kujifananisha nao kwenye ususuwavu wa nyoyo zao. Ugumu wa nyoyo ni kutokana na madhambi.”[2]

Ibn Kathiyr (Rahimahu Allaah) amesema:

”Kwa ajili hiyo Allaah akawakataza waumini kujifananisha nao katika mambo yao ya kimsingi na ya kitanzu.”[3]

[1] 57:16

[2] Iqtidhwaa’-us-Swiraat al-Mustaqiym, uk. 43

[3] Tafsiyr al-Qur-aan al-´Adhiym (4/396).

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Jilbaab-ul-Mar-ah al-Muslimah, uk. 163-164
  • Imechapishwa: 29/10/2023