102. Hapa ndipo waislamu hukosa ulinzi wa Allaah

Vilevile Amesema (Ta´ala):

وَالَّذِينَ آتَيْنَاهُمُ الْكِتَابَ يَفْرَحُونَ بِمَا أُنزِلَ إِلَيْكَ ۖ وَمِنَ الْأَحْزَابِ مَن يُنكِرُ بَعْضَهُ ۚ قُلْ إِنَّمَا أُمِرْتُ أَنْ أَعْبُدَ اللَّـهَ وَلَا أُشْرِكَ بِهِ ۚ إِلَيْهِ أَدْعُو وَإِلَيْهِ مَآبِ وَكَذَٰلِكَ أَنزَلْنَاهُ حُكْمًا عَرَبِيًّا ۚ وَلَئِنِ اتَّبَعْتَ أَهْوَاءَهُم بَعْدَ مَا جَاءَكَ مِنَ الْعِلْمِ مَا لَكَ مِنَ اللَّـهِ مِن وَلِيٍّ وَلَا وَاقٍ

”Na wale Tuliowapa Kitabu  wanafurahia kwa yale yaliyoteremshwa kwako. Lakini miongoni mwa makundi wako wanaoyapinga baadhi yake. Sema: ”Hakika mimi nimeamrishwa nimuabudu Allaah na nisimshirikishe. Kwake nalingania na Kwake ndio marejeo yangu.” Na namna hiyo ndivyo Tumeiteremsha hali ya kuwa ni hukumu kwa kiarabu. Na ikiwa utafuata matamanio yao, baada ya kukujia elimu, basi hutokuwa na mlinzi yeyote wala mwenye kukuhami mbele ya Allaah.”[1]

Dhamira ya ”matamanio yao” inarejea kwa wale watu waliyotajwa hapo mwanzo, nayo ni yale makundi yanayorudisha baadhi yake. Wanaingia ndani yake mayahudi, manaswara na kila anayepinga kitu katika Qur-aan. Amesema (Ta´ala):

وَلَئِنِ اتَّبَعْتَ أَهْوَاءَهُم بَعْدَ مَا جَاءَكَ مِنَ الْعِلْمِ مَا لَكَ مِنَ اللَّـهِ مِن وَلِيٍّ وَلَا وَاقٍ

”Na ikiwa utafuata matamanio yao, baada ya kukujia elimu, basi hutokuwa na mlinzi yeyote wala mwenye kukuhami mbele ya Allaah.”

Kuwafuata katika yale mambo maalum ya dini yao ni kuyafuata matamanio na tamaa zao. Bali kuyafuata matamanio yao kunapatikana kwa mambo madogo kuliko hayo.

[1] 13:36-37

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Jilbaab-ul-Mar-ah al-Muslimah, uk. 162-163
  • Imechapishwa: 29/10/2023