104. Thibitisha kwanza kuhusu yanayosemwa juu ya wanachuoni

Maneno yake:

“Sulaymaan bin Suwhaym imewafikieni.”

Huyu ni mmoja katika wapinzani wa Shaykh katika kipindi chake. Kimeambatana na Mi´kaal ambapo ni kitongoji Riyaadh kinachotambulika kwa jina hilo mpaka hii leo. Katika kitongoji hichi walikuwa wamekusanyika watu katika makhurafi akiwemo bwana huyu. Walikuwa wakimsemea uongo Shaykh na wakiandika vitabu vinavyowachekesha watu katika tuhuma na uongo wao. Shaykh amejibu uzushi wa Suwhaym katika kijitabu kilichomo ndani ya vitabu vya Shaykh na hapa ameashiria jambo hilo. Hapa kuna ishara peke yake. Vinginevyo ipo Radd ya upambanuzi katika kitabu cha kujitegemea juu ya Sulaymaan bin Suwhaym. Alimwandikia:

“Kutoka kwa Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab kwenda kwa Sulaymaan bin Suwhaym. Amma ba´d: Nimefikiwa na khabari kwamba wewe unasema moja mbili… “

Amejibu kila uzushi.

Maneno yake:

“… imewafikieni… ”

Ni kana kwamba amehisi (Rahimahu Allaah) kuulizwa na watu wa Qaswiym juu ya ´Aqiydah yake sababu yake ni barua ya Ibn Suwhaym. Walipofikiwa na barua ya Ibn Suwhaym ndio wakamwandikia Shaykh wakimuuliza ´Aqiydah yake. Huu ndio wajibu. Lililo la wajibu ni kuhakikisha. Walifanya vizuri katika jambo hili. Ukifikiwa na khabari kuhusu Shaykh kwamba anasema hivi na vile basi wajibu wako ni wewe kuhakikisha. Amesema (Ta´ala):

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِن جَاءَكُمْ فَاسِقٌ بِنَبَإٍ فَتَبَيَّنُوا

“Enyi walioamini! Anapokujieni fasiki kwa habari yoyote, basi pelelezeni… “

Bi maana thibitisheni.

أَن تُصِيبُوا قَوْمًا بِجَهَالَةٍ فَتُصْبِحُوا عَلَىٰ مَا فَعَلْتُمْ نَادِمِينَ

“… msije mkawasibu watu kwa ujinga, mkawa kuwa wenye kujuta juu ya ambayo mmeyafanya.”[1]

Laiti wanafunzi hii leo na vijana wangefuata mwenendo huu na wakathibitisha na wakaacha mambo haya ya migogoro na kuvutana kati yao. Kwa sababu ni ndugu na wanafunzi. ´Aqiydah yao ni moja. Wangeacha mizozo na tuhuma hizi na wakahakikisha juu ya yale yaliyoko baina yao. Kukithibiti kitu juu ya yale yaliyosemwa basi wanasihiane kati yao na wasilichukulie kulianika, kutuhumiana na kuzozana katika maneno. Kitendo hichi hakijuzu kabisa. Kilicho cha wajibu ni kuthibitisha kwanza. Kukithibiti basi anasihiwe yule ambaye kosa limethibiti kwake. Kwa sababu mtu hakukingwa na kukosea.

Yupo mtu mwingine anayeitwa ´Abdullaah bin Suwhaym katika wanafunzi wa Shaykh. Ni mtu ambaye ni mzuri. Kwa hiyo msichanganye kati ya ´Abdullaah bin Suwhaym na  Sulaymaan bin Suwhaym.

[1] 49:06

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Aqiydat-il-Imaam Mujaddid Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab, uk. 144-145
  • Imechapishwa: 03/06/2021