102. Hii niliyoandika ndio ´Aqiydah yangu kwa ufupi

Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

Hii ni ´Aqiydah kwa ufupi nimeiandika akili yangu ikiwa mashghuli ili msome kile kilicho kwangu – na Allaah kwa tuyasemayo ni mdhamini anayetegemewa kwa yote. Jengine ni kwamba nyote mnatambua kuwa nimefikiwa na khabari kwamba barua ya Sulaymaan bin Suwhaym imewafikieni na kwamba wameikubali na kuisadikisha baadhi ya wale wanaojinasibisha na elimu upande wenu.

MAELEZO

Anawazungumzisha watu wa Qaswiym waliomuuliza kuhusu ´Aqiydah yake hali ya kusema:

“Hii ni ´Aqiydah kwa ufupi nimeiandika akili yangu ikiwa mashghuli.”

Kwa sababu (Rahimahu Allaah) alikuwa ni mwenye kushughulishwa na kazi yake tukufu katika kulingania kwa Allaah na kufunza na mambo makubwa aliyoyafanya (Rahimahu Allaah). Kijitabu chake hichi kidogo ni jibu juu ya swali lao na upana wake unapatikana katika vitabu vya ´Aqiydah vilivyopambanua. Kwa mfano “al-´Aqiydah al-Waasitwiyyah”, “al-´Aqiydah at-Twahaawiyyah” na maelezo yavyo.

Maneno yake:

“… ili msome kile kilicho kwangu.”

Kwa sababu walimtuhumu mambo ambayo yeye yuko nayo mbali. Ndipo akaibainisha ´Aqiydah yake ili awaraddi wapinzani wake na awakadhibishe juu ya yale wanayosema juu yake (Rahimahu Allaah).

Maneno yake:

“Allaah kwa tuyasemayo ni mdhamini anayetegemewa kwa yote.”

Anamshuhudisha Allaah juu ya hayo. Hayo ni kutokana na ukweli wake (Rahimahu Allaah). Ni kama ambavo mwanzoni mwa ´Aqiydah amemshuhudisha Allaah, Malaika Wake na wale waumini waliokuwa pamoja naye juu ya yale yaliyomo ndani yake.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Aqiydat-il-Imaam Mujaddid Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab, uk. 142
  • Imechapishwa: 02/06/2021