Swali: Wiki iliyopita nilipewa jukumu la kuuliza swali kuhusu alama za barabarani zinazobeba ujumbe kama:

سبحان الله

”Allaah ametakasika kutokamana na mapungufu.”

الحمد لله

”Himdi zote njema anastahiki Allaah.”

Mtu mmoja katika sisi akasema: Je, si ni Bid´ah? Je, ni kitu kilichofanywa na Maswahabah? Ni kipi kigezo cha nini Bid´ah?

Jibu: Bid´ah ni mtu kumwabudu Allaah kwa mambo ambayo hakumuwekea nayo katika Shari´ah. Hii ndio Bid´ah. Kuhusu njia za ´ibaadah sio Bid´ah. Kuna tofauti kati ya malengo na njia. Kwa mfano mtu akisema kuwa ni Bid´ah kutumia vipaza sauti wakati wa kuswali, kutoa Khutbah na mawaidha, tutamwambia kuwa ni kosa. Kwa sababu vipaza sauti ni njia ya kuwafikishia watu kheri. Vibango vinavyopatikana barabarani ni njia ya kuwakumbusha watu kumtaja Allaah (´Azza wa Jall).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Liqaa’ al-Baab al-Maftuuh (25 B) Tarehe: 11:20
  • Imechapishwa: 02/06/2021