Swali: Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) alisema kumwambia Muusa:

فَقُولَا لَهُ قَوْلًا لَّيِّنًا لَّعَلَّهُ يَتَذَكَّرُ أَوْ يَخْشَىٰ

“Mwambieni maneno laini huenda akawaidhika au akaogopa.”[1]

Hata hivyo katika Suurah ”al-Israa´” tunaona kuwa Muusa alimwambia kwa ukali na ugumu. Kwa mfano Muusa alimwambia:

وَإِنِّي لَأَظُنُّكَ يَا فِرْعَوْنُ مَثْبُورًا

”Hakika mimi bila shaka nakuona, ee, Fir’awn, kuwa umeshaangamia.”[2]

Ni vipi tutaoanisha kati ya Aayah hii na mahimizo ya kufanya upole?

Jibu: Mosi alianza kwa kumzungumzisha kwa upole. Wakati alipochupa mpaka na akajikweza ndio akastahiki kutwezwa. Huu ni moja wa mfano wa kwenda hatua kwa hatua wakati wa kulingania kwa Allaah kwa hekima. Kwanza unatakiwa uzungumze na yule unayemlingania kwa upole na wepesi. Aking´ang´ania na kufanya ukaidi basi hakuna malipo yake mengine isipokuwa kufanyiw upole.

[1] 20:44

[2] 17:102

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Liqaa’ al-Baab al-Maftuuh (16 A) Tarehe: 27.05
  • Imechapishwa: 02/06/2021