Allaah (Subhaanah) amewawekea katika Shari´ah waja Wake kuswali swalah ya ´iyd, ambayo ni katika kukamilisha kumtaja Allaah (´Azza wa Jall). Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amewaamrisha ummah wake waume kwa wake. Amri yake ni yenye kutiiwa. Amesema (Ta´ala):

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا أَطِيعُوا اللَّـهَ وَأَطِيعُوا الرَّسُولَ وَلَا تُبْطِلُوا أَعْمَالَكُمْ

”Enyi walioamini! Mtiini Allaah na mtiini Mtume na wala msitengue matendo yenu.”[1]

Mtume amewaamrisha wanawake kutoka kwenda kuswali swalah ya ´iyd, licha ya kwamba nyumba ni bora kwao isingelikuwa hii swalah. Hii ni dalili juu ya kusisitizwa kwake. Umm ´Atwiyyah (Radhiya Allaahu ´anhaa) ameeleza:

“Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ametuamrisha kuwatoa katika [´Iyd] al-Fitwr na [´Iyd] al-Adhwhaa´; wanawali, wenye hedhi na wasichana mabikira. Ama wale wenye hedhi watajitenga na uwanja wa kuswalia na watashuhudia kheri na ulinganizi wa waislamu.” Nikasema: ”Ee Mtume wa Allaah, wakati mwingine mmoja wenu anakuwa hana jilbaab?” Akasema: ”Dada yake amvishe katika jilbaab zake.”

Ameipokea al-Bukhaariy na Muslim.

Jilbaab ni vazi ambalo mwanamke anajisitiri nalo sawa na ´Abaa´ah.

[1] 47:33

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majaalis Shahr Ramadhwaan, uk. 224-225
  • Imechapishwa: 28/03/2024