Saudi Arabia kutokana na tunavyojua ndio nchi bora kabisa katika kuitekeleza Shari´ah. Hili ni jambo lenye kushuhudiwa. Hatusemi kuwa ni yenye kukamilika kwa asilimia mia. Bali kuna mapungufu mengi. Kuna mambo ya dhuluma na mambo ya upendeleo. Lakini mambo hayo ya dhuluma ukiyalinganisha na uadilifu utaona kuwa ni madogo. Miongoni mwa dhuluma pia ni mtu kuyafumbia macho yale mazuri na akayaona yale mabaya peke yake. Mambo yakishakuwa hivo basi italazimika mtu ahukumu kwa uadilifu:

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا كُونُوا قَوَّامِينَ بِالْقِسْطِ شُهَدَاءَ لِلَّـهِ وَلَوْ عَلَىٰ أَنفُسِكُمْ أَوِ الْوَالِدَيْنِ وَالْأَقْرَبِينَ

“Enyi walioamini! Kuweni wasimamizi wa uadilifu mtoapo ushahidi kwa ajili ya Allaah japokuwa ni dhidi ya nafsi zenu au wazazi wawili au jamaa wa karibu.”[1]

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُواْ كُونُواْ قَوَّامِينَ لِلّهِ شُهَدَاء بِالْقِسْطِ وَلاَ يَجْرِمَنَّكُمْ شَنَآنُ قَوْمٍ عَلَى أَلاَّ تَعْدِلُواْ اعْدِلُواْ هُوَ أَقْرَبُ لِلتَّقْوَى وَاتَّقُواْ اللّهَ إِنَّ اللّهَ خَبِيرٌ بِمَا تَعْمَلُونَ

”Enyi walioamini! Kuweni wasimamizi madhubuti kwa ajili ya Allaah pindi mnapotoa ushahidi kwa uadilifu na wala chuki ya watu isikufanyeni kutokufanya uadilifu – fanyeni uadilifu – hivyo ni karibu zaidi na uchaji Allaah; hakika Allaah ni Mwenye khabari wa yote mnayoyafanya.”[2]

Kwa maana ya kwamba kuwachukia watu fulani kusikupelekeeni kutofanya uadilifu.

[1] 4:135

[2] 5:8

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Hujj al-Qawiyyah ´alaa Wujuub-id-Difaa´ ´an-id-Dawlah as-Su´uudiyyah, uk. 13-14
  • Imechapishwa: 28/03/2024