Allaah ameilinda nchi yetu kujenga juu ya makaburi. Hilo ni kutokana na fadhilah za Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) kisha kutokana na matunda ya ulinganizi mtukufu wa Salafiyyah ambao alisimama nao kiongozi wa Salafiyyah na mnusuru wa Salafiyyah: Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab na Muhammad bin Sa´uud. Allaah awarehemu na amrehemu kila ambaye amepita juu ya njia hiyo. Huwezi kupata nchi yetu watu wanajenga juu ya makaburi. Hilo ni katika upole na rehema za Allaah juu yetu.

  • Mhusika: ´Allaamah Swaalih bin Muhammad al-Luhaydaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Muhadhara: Haqiyqat-ul-Bay´ah fiyl-Islaam wa Bayaan Shuruutwihaa wa Khatwar Naz´ihaa
  • Imechapishwa: 28/03/2024