10. Mara kama nguruwe, mara kama mijibwa

Lau Shari´ah isingeharamisha unywaji pombe basi akili iliosalimika ingelikuwa ni hoja tosha kuonesha ubaya wake. Kwa sababu pombe inaondosha akili ambayo ndio yenye kumpambanua mwanadamu na wanyama. Hivyo kwa uchache chapombe anashuka kwenye ngazi ya wanyama. Utaona namna ambavyo baadhi ya watumiaji pombe wamezama kwenye najisi, machafu na matapishi – wamefanana na nguruwe. Baadhi ya wengine wakaua au wakawaumiza wengine – wamefanana na wanyama wakali kama mfano wa majibwa.

Ee chapombe! Kuwa mwangalifu juu ya jinai yake!

Wewe ni mtu mwenye akili ilihali pombe inafichua vilivojificha,

inaua akili na inapelekea madhambi huko Aakhirah

Kutokana na matokeo ya pombe wengi katika watu wa kipindi cha ujinga waliiharamisha kabla ya Uislamu. Baadhi yao wamesema:

“Kilevi kilikuja kwa kiumbe ambaye alikuwa mpendwa zaidi kwa Allaah kikamuharibu.”[1]

Bi maana akili.

Pengine mwendawazimu akawa na hali bora zaidi kuliko mlevi. Abu Ishaaq al-Fizaariy amesema:

“Nilimuona mwehu akipiga makelele akilingana na kichwa cha mlevi.”[2]

Sa´duun mwendawazimu alionekana akikaa karibu na kichwa cha mzee mlevi. Alipoulizwa sababu ya kufanya hivo akasema: “Huyu ni mwendawazimu.” Akaambiwa: “Wewe ndiye mwendawazimu au yeye?” Akasema: “Yeye ndiye mwendawazimu. Kwa sababu mimi nimeswali Dhuhr na ´Aswr katika mkusanyiko na yeye hakuswali si katika mkusanyiko wala peke yake. Akaulizwa kama ana shairi lolote juu ya hilo ambapo akajibu: “Ndio:

Nimeacha mvinyo kwa ajili ya wanywaji mvinyo

na nimekuwa ni mwenye kunywa maji masafi

Kwa sababu mvinyo unamdhalilisha mtukufu

na unazifanya nyuso nzuri kuwa mbaya[3]

[1] al-Bayhaqiy katika ”Shu´b-ul-Iymaan” (5602) kutoka kwa al-Hasan al-Baswriy.

[2] Ibn Abiyd-Dunyaa katika ”Dhamm-ul-Muskir”, uk. 75

[3] Tazama ”Swifat-us-Swafwah” (2/515) ya Ibn-ul-Jawziy.

  • Mhusika: Imaam Zayn-ud-Diyn bin Rajab al-Hanbaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Dhamm-ul-Khamr, uk. 21-23
  • Imechapishwa: 23/07/2020