5- Ni haramu kwa mwanamke mwenye hedhi kubaki msikitini. Bali ni haramu kwake kubaki hata mahali pa kuswalia ´Iyd. Umm ´Atwiyyah amesema:

“Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alituamrisha katika ´Iyd mbili kuwatoa wanawake chipukizi ambao ndio wametoka katika kukomaa, wanawake wenye hedhi na ambao hawajaolewa. Kuhusiana na wanawake wenye hedhi, waepuke sehemu za kuswalia.”[1]

[1] al-Bukhaariy (324) na Muslim (890).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ad-Dimaa’ at-Twabiy´iyyah lin-Nisaa’ http://www.ibnothaimeen.com/all/books/article
  • Imechapishwa: 30/10/2016