09. Suurah al-´Aswr imewasimamishia hoja viumbe

Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

ash-Shaafi´iy (Rahimahu Allaah) amesema:

“Lau Allaah asingeliteremsha hoja yoyote kwa viumbe Wake isipokuwa Suurah hii, basi ingeliwatosheleza.”[1]

MAELEZO

Hiyo ina maana ya kwamba lau kama Allaah asingewateremshia viumbe Wake hoja isipokuwa Suurah hii basi ingeliwatosha. Kwa sababu Suurah hii inawasimishia hoja. Imebainisha kuwa wenye kushinda ni wale wanaosifika na sifa hizi na kwamba mwenye kukosa sifa hizi amekhasirika.

Haina maana kuwa Suurah hii inawatosheleza katika kuyapambanua mambo ya Shari´ah. Ni lazima kuwepo upambanuzi ili zitambulike hukumu za swalah, hukumu za swawm, hukumu za hajj na mengineyo katika mambo ya ´ibaadah na miamala. Makusudio ya ash-Shaafi´iy (Rahimahu Allaah) ni kuwa ingeliwatosheleza katika kusimamisha hoja dhidi yao. Kwani Suurah hii  imemuwajibishia mtu kujifunza, kufanya matendo, kulingania na kufanya subira. Aidha imebainisha kuwa sifa hizi ndio za wale walioshinda na kwamba mwenye kuzikosa amekula khasara. Allaah, mbali na Suurah hii, ameteremsha Suurah hoja nyingi zisizohesabika ndani ya Qur-aan na Sunnah. Ibn Rajab (Rahimahu Allaah) amesema:

“Suurah hi ndio mizani ya matendo ambayo muumini anatakiwa kuyapima kwayo matendo yake. Kupitia Suurah hii atabainikiwa ima na kushinda au kula kwake khasara.”[2]

[1] Tazama ”Tafsiyr” (03/1461) ya ash-Shaafi´iy, ”Majmuu´-ul-Fataawaa” (28/152) ya Ibn Taymiyyah na ”Tafsiyr” (01/203) ya Ibn Kathiyr.

[2] Latwaaif-ul-Ma´aarif, uk. 300.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Thalaathat-il-Usuwl, uk. 22
  • Imechapishwa: 01/02/2023