09. Shungi za wanawake wa hapo kabla ya kuja Uislamu

Haafidhw Ibn-ul-Qattwaan amesema tena:

”Uelewa wetu kwamba udhahiri wa Aayah ni kuvuliwa uso na mikono unasapotiwa na maneno Yake:

وَلْيَضْرِبْنَ بِخُمُرِهِنَّ عَلَىٰ جُيُوبِهِنَّ

“Waangushe shungi zao mpaka vifuani mwao.”

Kinachopata kufahamika ni kwamba hereni zingeweza kuonekana wakati zinapofunuliwa nyuso zao. Kwa ajili hiyo ndio maana wakaamrishwa wajitupie mtandio vifuani mwao ili kusionekane kitu – isipokuwa uso na mikono ambavyo kikawaida ndio huonekana isipokuwa kama vitafunikwa kwa makusudi na kwa uzito.

Wafasiri wa Qur-aan wametaja kuwa sababu ya kuteremka kwa Aayah hiyo ni wanawake katika kipindi hicho walikuwa wanapofunika vichwa vyao basi mikia inashuka migongoni mwao, kama wanabataea, na hivyo shingo na vifua vyao vinabaki wazi. Ndipo Allaah (Subhaanah) akaamrisha kuteremsha mitandio juu ya vifua ili kifunikwe kila kitu. Amri hiyo ikafanyiwa kazi ipasavyo na wanawake wa Wahamaji na Wanusuraji na hivyo wakafunga sitara zao zaidi.”[1]

Kisha akataja Hadiyth inayokuja ya ´Aaishah kwa tamko la Abu Daawuud:

”Wakazikata shuka zao za chini na kuzitumia kama shungi.”[2]

[1] an-Nadhwar fiy Ahkaam-in-Nadhwar (2/21 – muswada).

[2] Amesema kuwa cheni ya wapokezi wake ni nzuri.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Jilbaab-ul-Mar-ah al-Muslimah, uk. 56
  • Imechapishwa: 04/09/2023