10. Kujiteremshia kwa mwanamke ndani ya Qur-aan kumeachiwa

Halafu Haafidhw Ibn-ul-Qattwaan (Rahimahu Allaah) akasema:

”Mtu akisema kuwa yale aliyoona juu ya kufaa kwa mwanamke kuonyesha uso na mikono yake yanapingana na maneno Yake (Ta´ala):

يَا أَيُّهَا النَّبِيُّ قُل لِّأَزْوَاجِكَ وَبَنَاتِكَ وَنِسَاء الْمُؤْمِنِينَ يُدْنِينَ عَلَيْهِنَّ مِن جَلَابِيبِهِنَّ ذَلِكَ أَدْنَى أَن يُعْرَفْنَ فَلَا يُؤْذَيْنَ وَكَانَ اللَّهُ غَفُورًا رَّحِيمًا

“Ee Nabii! Waambie wake zako na mabinti zako – na wanawake wa waumini – wajiteremshie Jilbaab zao; hivyo kunapeleka karibu zaidi watambulikane wasiudhiwe. Na Allaah daima ni Mwingi wa kusamehe, Mwenye kurehemu.”

nasema kuwa uteremshaji huu unaweza kufasiriwa kwa njia isiyopingana na yale tuliyosema. Maana yake ni kwamba wajiteremshie jilbaab zao kwa njia ya kwamba kusionekane mikufu na hereni zao. Ni kama mfano wa maneno Yake:

وَلْيَضْرِبْنَ بِخُمُرِهِنَّ عَلَىٰ جُيُوبِهِنَّ

“Waangushe shungi zao mpaka vifuani mwao.”

Ujiteremshiaji uliyoamrishwa ni kwa kuachia inapokuja kwa kila kinachoamrishwa kuteremshiwa. Pindi neno ”kuteremsha” litapotumiwa katika kila kitu ndipo hubainika kilichokusudiwa, kwa sababu Aayah haijaamrisha kukiteremshia kila kitu. Aayah ni kwa njia ya kuitikia na si makatazo na makanusho.”

Haya yanafahamisha kuwa maneno yake Haafidhw Ibn-ul-Qattwaan yanaafikiana kabisa na ijtihaad yangu juu ya kwamba Aayah haikufungamanishwa.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Jilbaab-ul-Mar-ah al-Muslimah, uk. 57
  • Imechapishwa: 04/09/2023