Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

jambo ambalo ni kumshirikisha Allaah. Allaah (Ta´ala) amesema juu yake:

إِنَّ اللَّـهَ لَا يَغْفِرُ أَن يُشْرَكَ بِهِ وَيَغْفِرُ مَا دُونَ ذَٰلِكَ لِمَن يَشَاءُ

“Hakikaha hasamehi kushirikishwa na anasamehe yaliyo chini ya hayo kwa Amtakae.”[1]

MAELEZO

Shirki inayaporomosha matendo. Amesema (Ta´ala):

وَلَقَدْ أُوحِيَ إِلَيْكَ وَإِلَى الَّذِينَ مِن قَبْلِكَ لَئِنْ أَشْرَكْتَ لَيَحْبَطَنَّ عَمَلُكَ وَلَتَكُونَنَّ مِنَ الْخَاسِرِينَ

“Hakika umefunuliwa Wahy na kwa wale walio kabla yako kwamba: “Ukifanya shirki bila shaka yataporomoka matendo yako na hakika utakuwa miongoni mwa waliokhasirika.”[2]

Shirki ndio dhambi kubwa, kitu kibaya kabisa na dhuluma kubwa mno. Atakayekutana na Allaah akiwa nayo basi Allaah hatomsamehe. Mwenye nayo atawekwa Motoni milele, jambo ambalo ni kubwa. Mja akishajua hivo basi analazimika kutilia umuhimu. Aidha anapaswa kuijua shirki na njia zake zinazomfikisha mtu huko. Sambamba na hayo amwombe Allaah amkinge kutokana na shirki. Allaah (Ta´ala) amesema kuhusu Ibraahiym:

وَاجْنُبْنِي وَبَنِيَّ أَن نَّعْبُدَ الْأَصْنَامَ

“Uniepushe mimi na wanangu kuabudu masanamu.”[3]

Bi maana niweke upande mmoja na masanamu haya upande mwingine na uweke kati yetu umbali mrefu. Ibraahiym ndiye ambaye alivunja masanamu na akawasusa watu wote. Akabaki peke yake mbele ya hawa makafiri. Allaah amesema juu yake:

إِنَّ إِبْرَاهِيمَ كَانَ أُمَّةً قَانِتًا لِّلَّـهِ حَنِيفًا وَلَمْ يَكُ مِنَ الْمُشْرِكِينَ

”Hakika Ibraahiym alikuwa ni mfano mwema, mnyenyekevu kwa Allaah na mwenye kuelemea Tawhiyd na kujiengua na shirki; hakuwa miongoni mwa washirikina.”[4]

Pamoja na hivyo anaogopa shirki na anaomba aepushwe na shirki.

Ibraahiym at-Taymiy (Rahimahu Allaah) amesema:

“Ni nani mwenye kujiaminisha na mtihani baada ya Ibraahiym?”[5]

Ikiwa Ibraahiym (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anaogopa shirki ni nani mwenye kujiaminisha baada yake?

Allaah (Ta´ala) amesema:

إِنَّ اللَّـهَ لَا يَغْفِرُ أَن يُشْرَكَ بِهِ وَيَغْفِرُ مَا دُونَ ذَٰلِكَ لِمَن يَشَاءُ

“Hakika Allaah hasamehi kushirikishwa lakini anasamehe yaliyo chini ya hayo kwa amtakae.”[6]

Ndani yake kuna ya kwamba shirki ni dhambi kubwa asiyoisamehe Allaah. Ambaye atakutana na Allaah akiwa nayo hatomsamehe. Kuhusu ambaye atakutana Naye akiwa na dhambi nyingine isiyokuwa shirki yuko chini ya utashi; Allaah akitaka kumsamehe atamsamehe kutokana na neema, fadhilah na ukarimu Wake, na akitaka kumuadhibu atamuadhibu kutokana na uadilifu Wake. Kwa ajili hiyo watenda madhambi yasiyokuwa shirki, ijapo watabaki Motoni kwa kipindi kirefu, baadaye watatoka. Hakuna wataodumishwa Motoni milele isipokuwa tu makafiri. Anayekufa juu ya shirki basi atadumishwa Motoni milele.

[1] 04:116

[2] 39:65

[3] 14:35

[4] 16:120

[5] Ibn Jariyr (17/17) na Ibn Abiy Haatim kama ilivyo katika ”ad-Durar al-Manthuur” (05/46).

[6] 04:48

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh al-Qawaa´id al-Arba´ah, uk. 127-128
  • Imechapishwa: 04/03/2023