08. Ndio maana ikawa ni muhimu mno kuzijua kanuni hizi nne

Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

Unapojua kuwa shirki inapoingia katika ´ibaadah inaiharibu na kubatilisha kitendo hicho na mwenye nayo anakuwa ni katika wataodumishwa Motoni milele, ndipo utaona kuwa suala hili ni muhimu sana kwa ulazima kulitambua. Huenda Allaah akakusalimisha na mtego huu,

MAELEZO

Ukishajua kuwa ´ibaadah inapochanganyika na shirki inaharibika na mwenye nayo anakuwa miongoni mwa watu wa Motoni na mwenye kuabudu masanamu, tena anakuwa miongoni mwa watu ambao watadumishwa Motoni milele. Ukishahakikisha jambo hilo basi inakuwa ni muhimu kwako kuijua nini Tawhiyd na ni nini shirki. Usichanganye haki na batili, Tawhiyd kwa shirki na ´ibaadah, ´ibaadah sahihi na ´ibaadah iliyoharibika. Huenda kwa kuyajua hayo Allaah akakuokoa na kukusalimisha kutokana na shirki.

Ikiwa Allaah hasamehi shirki, mwenye nayo atadumishwa Motoni milele na ameharamishiwa kuingia Pepo, basi hayo yanatakiwa kumfanya muislamu kutilia umuhimu jambo hili na atahadhari nayo ipasavyo. Anaweza kusalimika na mtego huo kwa kuzijua kanuni hizi nne ambazo zinapambanua kati ya mshirikina na mpwekeshaji. Ni kanuni zilizotajwa na Allaah ndani ya Kitabu Chake.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh al-Qawaa´id al-Arba´ah, uk. 126
  • Imechapishwa: 04/03/2023