09. Mke mwema anajihifadhi nafsi yake

3 – Anaihifadhi nafsi yake wakati ambapo mume wake anapokuwa mbali naye na heshima yake kutokana na mkono unaogusa, jicho linalotazama au sikio linalosikia. Vivyo hivyo anawahifadhi watoto, nyumba na mali za mume wake. Allaah (Ta´ala) amesema:

فَالصَّالِحَاتُ قَانِتَاتٌ حَافِظَاتٌ لِّلْغَيْبِ بِمَا حَفِظَ اللَّـهُ

“Basi wanawake wema ni wale watiifu wenye kujihifadhi katika hali ya kutokuweko waume zao kwa kuwa Allaah ameamrisha wajihifadhi.”[1]

as-Sa´diy amesema:

فَالصَّالِحَاتُ قَانِتَاتٌ

“Basi wanawake wema ni wale watiifu… “

Bi maana anayemtii Allaah (Ta´ala):

حَافِظَاتٌ لِّلْغَيْبِ

“… wenye kujihifadhi katika hali ya kutokuweko waume zao.”

Bi maana wanaowatii waume zao hata wakiwa hawapo. Anamuhifadhi mume wake kwa yeye kuichunga nafsi na mali yake.”[2]

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mwanamke akiswali vitano vyake, akafunga mwezi wake, akamtii mume wake na akahifadhi tupu yake, basi ataambiwa [siku ya Qiyaamah]: “Ingia Peponi kwa mlango wowote unaoutaka.”[3]

[1] 04:24

[2] Taysiyr-ul-Kariym ar-Rahmaan (01/344).

[3] Ibn Hibbaan katika ”as-Swahiyh” yake (06/184 – Ihsaan) na wengineo. al-Albaaniy ameisahihisha kutokana na nyinginezo zinazoitolea ushahidi katika “Aadab-uz-Ziffaaf”, uk. 286.

  • Mhusika: Shaykh Muhammad Shuwmaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swifaat-uz-Zawjah as-Swaalihah, uk. 23-24
  • Imechapishwa: 26/09/2022