Wale Mitume watano wenye subira sana ndio bora zaidi. Nao ni Nuuh, Ibraahiym, Muusa, ´Iysaa na Muhammad (Swalla Allaahu ´alayim wa sallam). Wametajwa katika maneno Yake (Ta´ala) katika Suurah al-Ahzaab:
وَإِذْ أَخَذْنَا مِنَ النَّبِيِّينَ مِيثَاقَهُمْ وَمِنكَ وَمِن نُّوحٍ وَإِبْرَاهِيمَ وَمُوسَىٰ وَعِيسَى ابْنِ مَرْيَمَ ۖ وَأَخَذْنَا مِنْهُم مِّيثَاقًا غَلِيظًا
“Na wakati Tulipochukua kutoka kwa Manabii fungamano lao, na kutoka kwako na kutoka kwa Nuuh na Ibraahiym na Muusa na ‘Iysaa mwana wa Maryam na Tukachukua kutoka kwao fungamano gumu.”[1]
Vilevile maneno Yake (Ta´ala) katika Suurah ash-Shuuraa:
شَرَعَ لَكُم مِّنَ الدِّينِ مَا وَصَّىٰ بِهِ نُوحًا وَالَّذِي أَوْحَيْنَا إِلَيْكَ وَمَا وَصَّيْنَا بِهِ إِبْرَاهِيمَ وَمُوسَىٰ وَعِيسَىٰ ۖ أَنْ أَقِيمُوا الدِّينَ وَلَا تَتَفَرَّقُوا فِيهِ ۚ
“Amekuwekeeni katika dini yale aliyomuusia kwayo Nuuh na ambayo tumekuteremshia Wahy wewe na tuliyomuusia kwayo Ibraahiym na Muusa na ‘Iysaa kwamba: “Simamisheni dini na wala msifarikiane humo.”[2]
Wabora katika hao watano ni wapenzi wa Allaah wa wandani; Ibraahiym na Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhim wa sallam). Mbora katika wawili hao ni Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Yeye ni sehemu yetu katika Mitume na sisi ni sehemu yake katika ummah wake. Kwa hivyo ni lazima kumuamini (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), kumshuhudilia ujumbe, kumtii katika maamrisho yake, kumsadikisha katika maelezo yake, kujiepusha na makatazo yake na aliyokemea na kumwabudu Allaah kwa yale aliyoyawekea Shari´ah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Aidha ni lazima kuamini kuwa yeye ndiye Mtume wa mwisho. Amesema (Ta´ala):
مَّا كَانَ مُحَمَّدٌ أَبَا أَحَدٍ مِّن رِّجَالِكُمْ وَلَـٰكِن رَّسُولَ اللَّـهِ وَخَاتَمَ النَّبِيِّينَ
“Hakuwa Muhammad baba wa yeyote miongoni mwa wanaume wenu, lakini ni Mtume wa Allaah na ni mwisho wa Manabii.”[3]
Imekuja katika Hadiyth ambayo ni Swahiyh:
“Utume umekhitimishwa kwangu.”[4]
[1] 33:07
[2] 42:13
[3] 33:40
[4] Muslim (523).
- Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Iymaan – Haqiyqatuhu wa Nawaaqidhwuh, uk. 16-17
- Imechapishwa: 21/03/2023
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)
Related
92. Mitume ndio viumbe bora
Imaam Ibn Qudaamah (Rahimahu Allaah) amesema: Muhammad ni Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´aalyhi wa sallam), ndiye Nabii wa mwisho na ndiye kiongozi wa Mitume. Imani ya mja haisihi mpaka aamini Ujumbe wake na ashuhudie utume wake. Watu hawatofanyiwa hesabu siku ya Qiyaamah isipokuwa baada ya uombezi wake. Hakuna Ummah…
In "Sharh Lum´at-il-I´tiqaad - Ibn ´Uthaymiyn"
62. Kuamini Mitume
Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema: ... Mitume Wake ... MAELEZO Mitume ni wingi wa “Mtume” na maana yake “mjumbe kwa ajili ya kufikisha kitu”. Makusudio hapa ya Mtume maana yake inakuwa “mtu aliyefunuliwa Wahy wa Shari´ah na akaamrisha kuufikisha”. Mtume wa kwanza alikuwa ni Nuuh na Mtume wa…
In "Sharh Thalaathat-il-Usuwl - Ibn ´Uthaymiyn"
08. Msingi wa nne ambao ni kuwaamini Mitume
Ni kuamini kwa kukata na kusadikisha ya kwamba Allaah (Ta´ala) ametumilizia watu Mitume na akawateremshia Wahy. Mitume hao wanawalingania watu na kuwaelekeza katika yale waliyoumbiwa kwayo ambayo ni kumwabudu Yeye pekee na kumtii. Aidha wanawabainishia njia ya uokozi na kuwahimiza kwayo na sambamba na hilo wanawatahadharisha na njia ya maangamivu.…
In "01. Tawhiyd-ur-Rubuubiyyah na maelezo yake"