Swali: Je, waliokufa wanahisi wale wanaowatembelea makaburini? Je, ni lazima kusimama mbele ya makaburi au inatosha peke yake kuingia makaburini?

Jibu: Allaah ndiye anayejua zaidi kuhusu maiti kuhisi anayemtembelea. Baadhi ya Salaf wamesema hivo. Lakini ni jambo halina dalili ya wazi kutokana na ninavojua. Lakini Sunnah ni yenye kutambulika kwa mujibu wa Shari´ah wakati wa kuyatembelea makaburi na kuwatolea salamu na kusema:

السلام عليكم دار قوم مؤمنين وإنا إن شاء الله بكم لاحقون نسأل الله لنا ولكم العافية يغفر الله لنا ولكم يرحم الله المستقدمين منا والمستأخرين

“Amani ya Allaah iwe juu yenu wakazi waumini na waislamu. Nasi – Allaah akitaka – tutaungana na nyinyi. Tunamuomba Allaah juu yetu sisi na nyinyi afya. Allaah akusameheni nyinyi na sisi. Allaah amrehemu aliyetangulia katika sisi na atakayekuja baadaye.”[1]

Yote haya yamewekwa katika Shari´ah. Kitendo cha kwamba anahisi au hahisi ni jambo linahitajia dalili ya wazi. Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) ndiye mjuzi zaidi. Lakini haitudhuru kitu kama wanahisi au hawahisi. Ni lazima kwetu kutekeleza Sunnah. Inatupendekeza kuyatembelea makaburi na kuwaombea du´aa ijapo wanahisi au hawatuhisi. Haya ni ujira kwetu na yanawafaa. Du´aa zetu kwao zinawafaa, matembezi yetu yanatufaa kwa sababu ndani yake kuna ujira, kukumbuka kifo na kukumbuka Aakhirah. Kwa hivo tunanufaika nayo. Maiti pia ananufaika kwa jambo hilo kwa sisi kumwombea du´aa, kumwombea msamaha na hivyo ananufaika kwa jambo hilo.

Kuhusu kusimama mbele ya kaburi ni wigo wake ni mpana. Akisimama mbele ya kaburi ni sawa na akisimama pembezoni na makaburi na akatoa salamu inatosha. Akisimama pembezoni mwa makaburi na akasema:

السلام عليكم أهل الديار من المؤمنين والمسلمين وإنا إن شاء الله بكم لاحقون نسأل الله لنا ولكم العافية يرحم الله المستقدمين منا والمستأخرين

“Amani ya Allaah iwe juu yenu wakazi waumini na waislamu. Nasi – Allaah akitaka – tutaungana na nyinyi. Tunamuomba Allaah juu yetu sisi na nyinyi afya. Allaah amrehemu aliyetangulia katika sisi na atakayekuja baadaye.”

inatosha. Akiwa karibu na kaburi la baba yake au kaburi la ndugu yake ndio bora na kamilifu zaidi. Akifika katika kaburi la ndugu yake, baba yake, jamaa yake au rafiki yake ambapo akasimama karibu naye na akasema:

السلام عليك يا فلان ورحمة الله وبركاته، غفر الله لك ورحمك الله، وضاعف حسناتك

“Amani, rehema na baraka za Allaah ziwe juu yako, ee fulani. Allaah akusamehe, akurehemu na akulipe maradufu matendo yako mema.”

au mfano wake ni jambo zuri. Hivi ndio bora na kamilifu zaidi.

[1] Muslim (974).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tahdhiyr min Fitnat-il-Qubuur, uk. 39-41
  • Imechapishwa: 12/04/2022