07. Aayah zinazojulisha juu ya kupwekeka Kwake

Ameelekeza (Subhaanah) ndani ya Kitabu Chake kitukufu juu ya hilo, akabainisha ya kwamba Yeye ndiye Mola wa walimwengu, akabainisha kuwa Yeye ndiye Mwingi wa kuumba, Mjuzi wa kila kitu, kwamba Yeye ndiye ameumba kila kitu na ya kwamba anainusuru haki. Amesimamisha dalili juu ya hayo maeneo mengi ndani ya Kitabu Chake ili aegemee juu yake yule anayetafuta haki. Amesema (Subhaanah):

وَإِلَـٰهُكُمْ إِلَـٰهٌ وَاحِدٌ ۖ لَّا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ الرَّحْمَـٰنُ الرَّحِيمُ

“Mungu wenu ni Mungu mmoja pekee; hapana mwabudiwa wa haki isipokuwa Yeye, Mwingi wa huruma, Mwenye kurehemu.”[1]

Amesema (Subhanaah) baada yake:

إِنَّ فِي خَلْقِ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَاخْتِلَافِ اللَّيْلِ وَالنَّهَارِ وَالْفُلْكِ الَّتِي تَجْرِي فِي الْبَحْرِ بِمَا يَنفَعُ النَّاسَ وَمَا أَنزَلَ اللَّـهُ مِنَ السَّمَاءِ مِن مَّاءٍ فَأَحْيَا بِهِ الْأَرْضَ بَعْدَ مَوْتِهَا وَبَثَّ فِيهَا مِن كُلِّ دَابَّةٍ وَتَصْرِيفِ الرِّيَاحِ وَالسَّحَابِ الْمُسَخَّرِ بَيْنَ السَّمَاءِ وَالْأَرْضِ لَآيَاتٍ لِّقَوْمٍ يَعْقِلُونَ

“Hakika katika kuumbwa mbingu na ardhi na kupishana usiku na mchana na merikebu zipitazo katika bahari viwafaavyo watu na aliyoteremsha Allaah kutoka mbinguni katika maji akahuisha kwavyo ardhi baada ya kufa kwake na akaeneza humo kila aina ya mnyama na mgeuko wa pepo na mawingu yanayotiishwa baina ya mbingu na ardhi ni alama kwa watu wenye akili.”[2]

Amesema (Tabaarak wa Ta´ala):

 يَا أَيُّهَا النَّاسُ اعْبُدُوا رَبَّكُمُ الَّذِي خَلَقَكُمْ وَالَّذِينَ مِن قَبْلِكُمْ لَعَلَّكُمْ تَتَّقُونَ الَّذِي جَعَلَ لَكُمُ الْأَرْضَ فِرَاشًا وَالسَّمَاءَ بِنَاءً وَأَنزَلَ مِنَ السَّمَاءِ مَاءً فَأَخْرَجَ بِهِ مِنَ الثَّمَرَاتِ رِزْقًا لَّكُمْ ۖ فَلَا تَجْعَلُوا لِلَّـهِ أَندَادًا وَأَنتُمْ تَعْلَمُونَ

“Enyi watu! Mwabuduni Mola wenu ambaye amekuumbeni na wale wa kabla yenu mpate kumcha. Ambaye amewafanyieni ardhi kuwa ni tandiko na mbingu kuwa ni paa na akateremsha kutoka mbinguni maji, akawatolea kwayo matunda kuwa ni riziki zenu. Hivyo basi, msimfanyie Allaah waliolingana naye na hali ya kuwa nyinyi mnajua.”[3]

إِنَّمَا إِلَـٰهُكُمُ اللَّـهُ الَّذِي لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ ۚ وَسِعَ كُلَّ شَيْءٍ عِلْمًا

”Hakika si venginevyo Mungu wenu ni Allaah ambaye hapana mwabudiwa wa haki isipokuwa Yeye. Amekienea kila kitu kwa elimu Yake.”[4]

وَقَضَىٰ رَبُّكَ أَلَّا تَعْبُدُوا إِلَّا إِيَّاهُ

“Mola wako ameamuru kwamba: “Msiabudu yeyote isipokuwa Yeye pekee.”[5]

إِيَّاكَ نَعْبُدُ وَإِيَّاكَ نَسْتَعِينُ

“Wewe pekee ndiye tunakuabudu na Wewe pekee ndiye tunakuomba msaada.”[6]

Zipo Aayah nyenginezo nyingi anazoelekeza (Subhaanah) ya kwamba Yeye ndiye Mola wa viumbe, Mola wa walimwengu na kwamba Mitume wamekuja na ujumbe huo. Amesema (Jalla wa ´Alaa):

وَلَقَدْ بَعَثْنَا فِي كُلِّ أُمَّةٍ رَّسُولًا أَنِ اعْبُدُوا اللَّـهَ وَاجْتَنِبُوا الطَّاغُوتَ

”Hakika Tulituma katika kila ummah Mtume kwamba: “Mwabuduni Allaah na jiepusheni na Twaaghuut [waungu batili].”[7]

وَمَا أَرْسَلْنَا مِن قَبْلِكَ مِن رَّسُولٍ إِلَّا نُوحِي إِلَيْهِ أَنَّهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا أَنَا فَاعْبُدُونِ

“Hatukutuma kabla yako Mtume yeyote isipokuwa Tulimfunulia Wahy ya kwamba: “Hakika hapana mwabudiwa wa haki isipokuwa Mimi; hivyo basi niabuduni.”[8]

ذَٰلِكَ بِأَنَّ اللَّـهَ هُوَ الْحَقُّ وَأَنَّ مَا يَدْعُونَ مِن دُونِهِ هُوَ الْبَاطِلُ وَأَنَّ اللَّـهَ هُوَ الْعَلِيُّ الْكَبِيرُ

“Hivyo ni kwa kuwa Allaah ndiye wa haki na kwamba vile wanavyoomba badala Yake ndiyo batili na kwamba Allaah ndiye Aliye juu kabisa, Mkubwa.”[9]

فَاعْبُدِ اللَّـهَ مُخْلِصًا لَّهُ الدِّينَ أَلَا لِلَّـهِ الدِّينُ الْخَالِصُ

“Mwabudu Allaah hali ya kumtakasia Yeye dini. Zindukeni! Ni ya Allaah pekee dini iliyotakasika.”[10]

اللَّـهُ خَالِقُ كُلِّ شَيْءٍ ۖ وَهُوَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ وَكِيلٌ

”Allaah ni Muumbaji wa kila jambo, Naye juu ya kila jambo ni mdhamini.”[11]

هَلْ مِنْ خَالِقٍ غَيْرُ اللَّـهِ

”Je, kuna muumbaji mwingine badala ya Allaah?”[12]

[1] 02:163

[2] 02:164

[3] 02:21-22

[4] 20:98

[5] 17:23

[6] 01:05

[7] 16:36

[8] 21:25

[9] 22:62

[10] 39:02-03

[11] 39:62

[12] 35:03

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahamiyyat-ul-´Ilm https://binbaz.org.sa/discussions/33/اهمية-العلم-في-محاربة-الافكار-الهدامة
  • Imechapishwa: 12/04/2022