08. Muumbaji pekee ndiye anastahiki kuabudiwa

Kisha akabainisha dalili katika maeneo mengi. Pindi muumini anapozingatia ataona kuwa dalili za kinakili zinatiliwa nguvu na dalili za kiakili zinazoshuhudiwa na zinazohisiwa. Kwa ajili hii akataja (Subhaanah) baada ya kusema:

يَا أَيُّهَا النَّاسُ اعْبُدُوا رَبَّكُمُ

“Enyi watu! Mwabuduni Mola wenu… “

Akasema hoja ya hilo akasema:

وَالَّذِينَ مِن قَبْلِكُمْ لَعَلَّكُمْ تَتَّقُونَ الَّذِي جَعَلَ لَكُمُ الْأَرْضَ فِرَاشًا وَالسَّمَاءَ بِنَاءً وَأَنزَلَ مِنَ السَّمَاءِ مَاءً فَأَخْرَجَ بِهِ مِنَ الثَّمَرَاتِ رِزْقًا لَّكُمْ ۖ فَلَا تَجْعَلُوا لِلَّـهِ أَندَادًا وَأَنتُمْ تَعْلَمُونَ

“… ambaye amekuumbeni na wale wa kabla yenu mpate kumcha. Ambaye amewafanyieni ardhi kuwa ni tandiko na mbingu kuwa ni paa na akateremsha kutoka mbinguni maji, akawatolea kwayo matunda kuwa ni riziki zenu. Hivyo basi, msimfanyie Allaah waliolingana naye na hali ya kuwa nyinyi mnajua.”[1]

Maana ni kwamba huyu Aliyetuumba ndiye anastahiki kumwabudu kwa sababu Yeye ndiye katuumba na jengine Yeye anachunga manufaa ya waja. Hili ni jambo linalotambulika kwa maumbile yaliyosalimika na akili sahihi. Hao hawakujiumba nafsi zao wameumbwa na Muumbaji wao. Allaah ndiye Muumbaji kwa dalili za kiakili na za kinakili. Kisha akasema (Subhaanah):

الَّذِي جَعَلَ لَكُمُ الْأَرْضَ فِرَاشًا وَالسَّمَاءَ بِنَاءً وَأَنزَلَ مِنَ السَّمَاءِ مَاءً فَأَخْرَجَ بِهِ مِنَ الثَّمَرَاتِ رِزْقًا لَّكُمْ ۖ فَلَا تَجْعَلُوا لِلَّـهِ أَندَادًا وَأَنتُمْ تَعْلَمُونَ

“Ambaye amewafanyieni ardhi kuwa ni tandiko na mbingu kuwa ni paa na akateremsha kutoka mbinguni maji, akawatolea kwayo matunda kuwa ni riziki zenu. Hivyo basi, msimfanyie Allaah waliolingana naye na hali ya kuwa nyinyi mnajua.”

Akabainisha (Subhaahahu wa Ta´ala) ni namna gani utafahamu vitu hivi vinavoonekana na vilivyoumbwa vinavofahamika na akili na kila mtu. Akatufanyia ardhi kuwa tandiko ambalo tunalala juu yake, tunatembea juu yake, tunachunga mifugo yetu juu yake, tunabeba juu yake, tunapanda juu yake miti, tunachukua madini kutoka ndani yake na mengineyo. Kisha akateremsha maji juu kutoka mawinguni. Ameteremsha mvua ambapo akatutolea matunda. Ni nani ambaye ameteremsha mvua? Ni nani ambaye ametoa matunda haya ambayo yanaliwa na watu na mimea waliyopanda na ambayo hawakupanda? Yote hayo ni kutokana na alama tukufu ya Allaah inayojulisha juu ya uwezo Wake mkubwa na kwamba Yeye ndiye Mola wa walimwengu.

Ardhi tulivu iliyofanywa imara kwa milima, akaitengenezea vigingi na akaifanya kuwa ni laini na tulivu tukapata kuishi juu yake. Sisi pia, vipanda vyetu kukiwemo magari yetu, sisi, wanayama wetu tunapata utulivu juu yake. Ndege zetu zinaruka juu ya anga yake. Tunaburudika kwa yale yote ambayo yameumbwa juu yake.

Vivyo hivyo mbingu imeumbwa juu yetu na ikapambwa kwa sayari na  nyota zinazokwenda na zilizosimama, ikawekwa jua na mwezi ili kuwatambuza viumbe uwezo wa Muumba Mkuu na Aliye juu, Mkubwa kabisa ambaye hana mshirika katika hayo (Subhaanahu wa Ta´ala).

[1] 02:21-22

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahamiyyat-ul-´Ilm https://binbaz.org.sa/discussions/33/اهمية-العلم-في-محاربة-الافكار-الهدامة
  • Imechapishwa: 12/04/2022