Isitoshe mazao haya mengi na matunda mbalimbali ambayo yana manufaa na maslahi mengi  pamoja na kutofautiana kwa rangi, aina, ukubwa, ladha, manufaa yake na mengineyo, hapo ndipo kutadhihiri uwezo wa Allaah (Subhaanah) na kustahiki Kwake kuabudiwa. Amesema (´Azza wa Jall):

وَإِلَـٰهُكُمْ إِلَـٰهٌ وَاحِدٌ ۖ لَّا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ الرَّحْمَـٰنُ الرَّحِيمُ إِنَّ فِي خَلْقِ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَاخْتِلَافِ اللَّيْلِ وَالنَّهَارِ وَالْفُلْكِ الَّتِي تَجْرِي فِي الْبَحْرِ بِمَا يَنفَعُ النَّاسَ وَمَا أَنزَلَ اللَّـهُ مِنَ السَّمَاءِ مِن مَّاءٍ فَأَحْيَا بِهِ الْأَرْضَ بَعْدَ مَوْتِهَا وَبَثَّ فِيهَا مِن كُلِّ دَابَّةٍ وَتَصْرِيفِ الرِّيَاحِ وَالسَّحَابِ الْمُسَخَّرِ بَيْنَ السَّمَاءِ وَالْأَرْضِ لَآيَاتٍ لِّقَوْمٍ يَعْقِلُونَ

“Mungu wenu ni Mungu mmoja pekee; hapana mwabudiwa wa haki isipokuwa Yeye, Mwingi wa huruma, Mwenye kurehemu. Hakika katika kuumbwa mbingu na ardhi na mabadiliko ya usiku na mchana na merikebu zipitazo kwenye bahari kwa vile viwafaavyo watu na aliyoyateremsha Allaah kutoka mbinguni katika maji ambapo akahuisha kwayo ardhi baada ya kufa kwake na akaeneza humo kila aina ya mnyama na kugeuka kwa upepo na mawingu yanayotiishwa kati ya mbingu na ardhi ni alama kwa watu wenye akili.”[1]

Yeye (Subhaanah) anatubainisha katika Aayah na alama hizi ambazo tunazishuhudia, kuziona na kuzihisi:

إِنَّ فِي خَلْقِ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَاخْتِلَافِ اللَّيْلِ وَالنَّهَارِ

“Hakika katika kuumbwa mbingu na ardhi na mabadiliko ya usiku na mchana.”[2]

Mbingu hizi, pamoja na upana na kurefuka kwake na yale mambo ya ajabu yaliyomo ndani yake. Ardhi hizi, pamoja na upana na kutandaa kwake, na ile mito, milima na venginevyo vilivyomo juu yake. Aidha kutofautiana kwa usiku na mchana na yale maji yanayoteremka kutoka juu mbinguni na vile vinavyotoka baharini katika vitu ambavyo vinawanufaisha watu na zile meli zinazobebwa na maji yake ambazo zinashikiliwa na maji haya. Meli ambazo zinabeba mahitajio mbalimbali ya watu na kuwabeba kuwatoa nchi moja hadi nyingine. Kisha kukateremshwa maji juu mbinguni ambayo yakaihuisha ardhi baada ya kufa kwake akaeneza humo kila aina ya mnyama na kugeuka kwa upepo na mawingu yanayotiishwa kati ya mbingu na ardhi.

Yule anayezingatia Aayah na alama hizi tukufu zinamwelekeza katika kuwepo kwa Muumba Wake ambaye ameziumba baada ya kutokuwepo kwake na kwamba Yeye ndiye Mola wa walimwengu (Subhaanahu wa Ta´ala) na kwamba viumbe hizi haviwezi kusimama isipokuwa kwa uwezo Wake (Subhaanah). Amesema (´Azza wa Jall):

وَمِنْ آيَاتِهِ أَن تَقُومَ السَّمَاءُ وَالْأَرْضُ بِأَمْرِهِ

“Miongoni mwa alama Zake, ni kwamba mbingu na ardhi zimesimama kwa amri Yake kisha.”[3]

Aayah hizi tunazozisoma na dalili tunazoziona na kuzitambua wanaonufaika kwazo ni wale wenye akili iliosalimika na macho yalionyooka. Kwa ajili hii akasema (Subhaanah) mwishoni mwa Aayah:

لَآيَاتٍ لِّقَوْمٍ يَعْقِلُونَ

“Ni ishara kwa watu wenye akili.”[4]

[1] 02:163-164

[2] 02:163-164

[3] 30:25

[4] 02:164

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahamiyyat-ul-´Ilm https://binbaz.org.sa/discussions/33/اهمية-العلم-في-محاربة-الافكار-الهدامة
  • Imechapishwa: 12/04/2022