Kuhalalisha Kwake (Ta´ala) kula na kunywa mpaka kuchomoza kwa alfajiri kuna dalili juu ya mapendekezo ya kula daku. al-Bukhaariy na Muslim wamepokea kupitia kwa Anas ambaye ameeleza kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Kuleni daku. Kwani hakika katika kula daku kuna baraka.”[1]

Kumepokelewa mapokezi mengi juu ya mahimizo ya kula daku ijapo ni kwa glasi ya maji. Kunapendekezwa mtu aicheleweshe mpaka ule wakati wa mwishomwisho wa alfajiri.

Endapo mtu ataamka na huku yuko na josho la janaba au ndio punde amesafika kutoka katika hedhi kabla ya kuchomoza kwa alfajiri, basi aanze kula daku na afunge. Acheleweshe kuoga mpaka baada ya kuchomoza kwa alfajiri.

[1] al-Bukhaariy (1923) na Muslim (2544).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Mulakhasw al-Fiqh (01/379)
  • Imechapishwa: 30/03/2021