Baadhi ya watu huamka mapema kula daku kwa sababu wanakesha sehemu kubwa ya usiku kisha baada ya hapo wanakula daku na wanalala masaa kadhaa kabla ya alfajiri. Hakika watu hawa wamefanya makosa mengi:

1- Wameanza kufunga kabla ya kuanza wakati wa kufunga.

2- Wanaacha kuswali fajr pamoja na mkusanyiko. Hivyo wanakuwa ni wenye kumuasi Allaah kwa kuacha swalah ya mkusanyiko aliyowawajibishia.

3- Pengine wakaichelewesha swalah ya fajr kutoka ndani ya wakati wake. Hivyo hawaiswali isipokuwa baada ya kuchomoza kwa alfajri, jambo ambalo ni jarima na dhambi kubwa. Allaah (Ta´ala) amesema:

فَوَيْلٌ لِّلْمُصَلِّينَ الَّذِينَ هُمْ عَن صَلَاتِهِمْ سَاهُونَ

“Ole wao waswaliji, ambao wanapuuza swalah zao.”[1]

[1] 107:04-05

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Mulakhasw al-Fiqh (01/380)
  • Imechapishwa: 30/03/2021