09. Kiongozi wa ulimwengu katika mavazi yaliyotiwa kiraka

35 – Ishaaq bin Ismaa´iyl ametuhadithia: Qabiyswah ametuhadithia: Sufyaan ametuhadithia, kutoka kwa ´Uqbah al-Asdiy, ambaye amesema:

”Ibraahiym aliletewa Khabiysw[1], akakataa kukila na akasema: ”Hiki ni chakula cha watoto.”

36 – ´Abdullaah bin Yuunus bin Bukayr ametuhadithia: Baba yangu amenihadithia: al-Hasan bin Diynaar ametuhadithia, kutoka kwa al-Hasan, kutoka kwa al-Ahnaf bin Qays, ambaye amesema:

”Tulitoka kama wajumbe na Abu Muusa al-Ash´ariy kwenda kwa ´Umar bin al-Khattwaab. ´Umar alikuwa na mikate mitatu. Siku moja anakula mkate kwa maziwa na siagi, siku ya pili kwa nyama safi na siku ya tatu kwa mafuta. Watu wakawa wanakula na kujipa udhuru, ambapo ´Umar akasema: ”Mimi nasikia kutoa kwenu nyudhuru. Hakuna kati yenu anayejua maisha zaidi kunishinda. Ningelitaka, basi ningeweza kula nyama laini, mafuta, nyama zilizochomwa, nyama za kukaanga na nyama zilizokaushwa, lakini nayahifadhi mema yangu. Allaah (Jalla wa ´Alaa) amewataja watu akasema:

أَذْهَبْتُمْ طَيِّبَاتِكُمْ فِي حَيَاتِكُمُ الدُّنْيَا وَاسْتَمْتَعْتُم بِهَا

”Je, mshamaliza vizuri vyenu katika uhai wenu wa dunia na mshajistarehesha navyo?”[2]

37 – ´Abdullaah bin Yuunus amenihadithia: Baba yangu amenihadithia: Abu Ma´shar amenihadithia, kutoka kwa Muhammad bin Qays, ambaye amesema:

”Jopo la watu waliingia kwa Hafswah bint ´Umar wakasema: ”Hakika mshipa wa shingo wa kiongozi wa waumini unaonekana kutokana na unyonge. Je, unaweza kumzungumzisha na kumuomba ale chakula bora zaidi kuliko anachokula na avae mavazi mazuri zaidi kuliko mavazi anayovaa? Tunamuona namna ambavyo kikoi chake kimetiwa viraka. Je, unaweza kumuomba alale kwenye godoro zuri zaidi kuliko analolalia? Kwani Allaah amewatajirisha waumini. Kwa njia hiyo atawatawala waislamu kirahisi zaidi. Wakamtuma Hafswah kwake na akawaeleza waliyosema. Akasema: ”Nieleze godoro zuri ulilomtandikia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallamm).” Akasema: ”Kitambaa kilichokunjwa sehemu mbili. Wakati kilipokuwa kigumu kukilalia, namkunjia nacho mara nne.” Akasema: ”Nieleze kuhusu nguo yake nzuri zaidi aliyovaa?” Akasema: ”Kitambaa cheusi tulichomshonea. Wakati mtu alipokuwa anakiona, anamuomba nacho, ambapo anampa nacho.” Akasema: ”Nipe pishi nane za tende.” Akawaamrisha kung´oa punje ambapo akasema: ”Ondoa maganda yake.” Wakafanya alichokisema. Kisha anala zote na kusema: ”Naapa kwa Allaah! Mimi natamani chakula. Mimi nakula siagi lakini niko na nyama. Nala mafuta lakini niko na nyama. Nala chumvi lakini niko na mafuta. Nala mkate lakini niko na chumvi. Lakini nachelea kupinda kutokamana na ile njia ambayo walipita juu yake marafiki zangu wawili.”

[1] Tamtam iliyotengenezwa kwa tende na siagi. 

[2] 46:20

  • Mhusika: Imaam Abu Bakr ´Abdullaah bin Muhammad bin Abiyd-Dunyaa
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-ul-Juu´, uk. 49-52
  • Imechapishwa: 19/06/2023