Unilinde kutokamana na shari kwa yale Uliyohukumu – Allaah anahukumu ya kheri kama ambavo anahukumu ya shari pia.

Kuhukumu Kwake ya kheri ni kheri tupu kwa kile kilichohukumiwa na yule aliyehukumiwa. Mfano wa hukumu ya kheri ni watu waandikiwe riziki kunjufu, amani, utulivu, uongofu na kupata nusura. Hii ni kheri kwa kile kilichohukumiwa na yule aliyehukumiwa.

Kuhukumu Kwake ya shari ni kheri katika ile hukumu na ni shari kwa yule muhukumiwaji. Mfano wa hilo ni ukame (kutonyesha mvua), jambo ambalo ni shari. Lakini ni kheri kule Allaah kuhukumu jambo hilo. Kivipi? Pengine mtu akahoji ni vipi inakuwa kheri pale Allaah anapotukadiria ukame na matokeo yake wanyama wanakufa na mazao yanaharibika? Sikiliza maneno ya Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala):

ظَهَرَ الْفَسَادُ فِي الْبَرِّ وَالْبَحْرِ بِمَا كَسَبَتْ أَيْدِي النَّاسِ لِيُذِيقَهُم بَعْضَ الَّذِي عَمِلُوا لَعَلَّهُمْ يَرْجِعُونَ

“Ufisadi umedhihiri katika nchi kavu na baharini kwa sababu ya yale iliyochuma mikono ya watu ili awaonjeshe baadhi ya ambayo wameyatenda ili wapate kurejea.”[1]

Kwa hivyo hukumu hii ina kusudio lenye kusifiwa. Kusudio lenyewe ni kule kujirejea kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) kwa njia ya kwamba mtu akaacha kumuasi na badala yake akamtii. Matokeo yake inakuwa ni shari kwa muhukumiwaji mwenyewe lakini hukumu yenyewe kama yenyewe inakuwa ni kheri.

Kwa hivyo maana ya:

”Unilinde kutokamana na shari kwa (ما)  yale Uliyohukumu.”

nilinde na shari Uliyohukumu. Allaah anahukumu shari kutokana na hekima kubwa na yenye kusifiwa. Haina maana ya shari ya hukumu Yako, hata hivyo maana yake ni shari ambayo. Kwa sababu hakuna shari katika hukumu Zake Allaah. Kwa ajili hiyo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema katika yale aliyomsifu Mola Wake:

والخير بيديك والشر ليس إليك

”Kheri zote ziko Mikononi Mwako. Shari haitoki Kwako.”

Kutokana na hayo shari hainasibishwi kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala).

[1] 30:41

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Du´aa´ al-Qunuut-il-Witr, uk. 13-15
  • Imechapishwa: 09/03/2024