Kwani hakika Wewe ndiye mwenye kuhukumu na wala Huhukumiwi – Allaah (´Azza wa Jall) anahukumu hukumu za Kishari´ah na hukumu za kilimwengu. Allaah (Ta´ala) anahukumu kwa kila kitu na kwa kila kitu, kwa sababu Yeye ndiye mwenye kuhukumu na hukumu kamili na yenye kuenea.

”… na wala Huhukumiwi.”

Kwa maana ya kwamba hakuna yeyote awezaye kumuhukumu. Waja hawawezi kumuhukumu Allaah, lakini Allaah ndiye anayewahukumu. Waja wataulizwa juu ya yale waliyoyafanya, lakini Allaah haulizwi:

لَا يُسْأَلُ عَمَّا يَفْعَلُ وَهُمْ يُسْأَلُونَ

“Haulizwi kwa yale Anayoyafanya, lakini wao wataulizwa.”[1]

[1] 21:23

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Du´aa´ al-Qunuut-il-Witr, uk. 15
  • Imechapishwa: 09/03/2024