Swali: Kuna mwanamke ambaye ametwahirika kabla ya alfajiri na hakuoga isipokuwa baada ya kuchomoza kwa jua. Analazimika kufunga?

Jibu: Ikiwa damu imekatika kabla ya kuchomoza kwa alfajiri basi atalazimika kujizuia na kufunga ijapo atachelewesha kuoga. Lakini haijuzu kwake kusubiri mpaka jua lichomoze. Bali antakiwa kuoga papo hapo pale tu damu yake itapokatika ili aweze kuswali swalah ya Fajr ndani ya wakati wake. Haijuzu kwake kuchelewesha kuoga mpaka jua likachomoza.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah Aalush-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Min Fataawaas-Swiyaam, uk. 18
  • Imechapishwa: 19/03/2022