Swali: Je, kuna alfajiri mbili, ya kweli na ya uwongo? Ni zipi alama zake?

Jibu: Alfajiri ya uwongo inakuwa ya usawa, inayotanda kuanzia mashariki kwenda magharibi na huitwa mwanga wa zodiacal. Alfajiri ya kweli inakuwa baada yake na huenea kuanzia kusini kwenda kaskazini. Mwanga wake huongezeka kwa wakati tofauti na alfajiri ya uwongo. Alfajiri ya wongo inakuwa ya usawa, yenye kufunikwa na giza na hupungua baada ya muda mfupi.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah Aalush-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Min Fataawaas-Swiyaam, uk. 18
  • Imechapishwa: 19/03/2022