Swali: Kuna mwanamke ambaye haswali isipokuwa katika Ramadhaan na katika baadhi ya masiku. Lakini hata hivyo anatoa swadaqah na anawasaidia wahitaji. Je, ambaye anaacha baadhi ya faradhi anakuwa kafiri na anatoka nje ya dini? Je, mwanamke huyu anasamehewa kwa matendo yake mema? Je, tule katika chakula chake?

Jibu: Kuswali kwake Ramadhaan pekee na kuacha kwake swalah nje ya Ramadhaan ni dalili ya unyonge wa imani moyoni mwake. Kitendo cha kupitikiwa na mwezi mzima haswali na anatosheka na kuswali katika Ramadhaan pekee ni dalili ya ujinga wake, uchache wa imani yake na kumwogopa kwake Allaah (Ta´ala). Ni lazima kwake kuswali kwa ajili ya Allaah katika miezi yote ndani ya Ramadhaan na nje yake. Kuacha kwake nje ya Ramadhaan ni jambo la khatari mno. Wako wanazuoni wenye kuona kuwa ambaye anaacha swalah kwa makusudi mpaka ukatoka nje wakati wake basi anakufuru kwa jambo hilo. Hali yake ni ya khatari. Ni lazima kwake kutubu kwa Allaah na achunge swalah zote. Swadaqah na matendo yake mema havimnufaishi kitu ikiwa anazembea juu ya swalah.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah Aalush-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Min Fataawaas-Swiyaam, uk. 18
  • Imechapishwa: 19/03/2022