08. Kutoka Jeddah kwenda Makkah kuswali Tarawiyh


Swali 8: Ni ipi hukumu watu wa Jeddah kwenda Makkah[1] kuswali Tarawiyh?

Jibu: Hakuna neno mtu akaenda katika msikiti Mtakatifu ili aswali Tarawiyh. Kwa sababu msikiti Mtakatifu ni miongoni mwa ile misikiti ambayo inafaa kufungiwa safari. Lakini ikiwa mtu ni mwajiriwa au ni imamu msikitini basi asiache kazi au akaacha uimamu kwa ajili ya kwenda katika msikiti Mtakatifu. Kwa sababu kuswali katika msikiti Mtakatifu ni jambo limependekezwa. Ama kutekeleza uwajibu wa kazi ni jambo la lazima. Haiyumkiniki kuacha jambo la lazima kwa ajili ya kufanya jambo lililopendekezwa.

Nimefikiwa na khabari kwamba baadhi ya maimamu wanaiacha misikiti yao na wanaenda Makkah kwa ajili ya kufanya I´tikaaf katika msikiti Mtakatifu au kwa ajili ya kuswali Tarawiyh. Hili ni jambo la kimakosa. Kwa sababu kutekeleza jambo la wajibu ni lazima na kwenda Makkah kuswali Tarawiyh au kukaa I´tikaaf si jambo la lazima.

[1] Takriban 80 km.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: 48 mas-alatu fiy Swiyaam, uk. 14
  • Imechapishwa: 11/04/2021