09. Kwenda katika misikiti ya mbali ambayo imamu anasoma vizuri

Swali 9: Ni ipi hukumu ya kuwafuata maimamu wenye sauti nzuri?

Jibu: Naona hakuna ubaya kufanya hivo. Lakini lililo bora ni mtu kuswali katika msikiti wake ili watu wakusanyike kwa imamu na kwenye msikiti wao. Jengine ili misikiti isikose watu. Sababu nyingine ni ili kusiwe na msongamano mkubwa katika msikiti ambao kisomo cha imamu wake ni kizuri na hivyo kukazuka mkanganyiko na pengine hata kukazuka jambo linalochukizwa. Pengine mtu akamkaba mwanamke anayetoka katika msikiti huu ambao una watu wengi. Kutokana na watu wengi na msongamano huenda hata akamteka nyara na mwanamke huyu asihisi hilo isipokuwa baada ya mwendo mrefu.

Kwa ajili hii naona kuwa mtu abaki katika msikiti wake kutokana na yale yanayopatikana ndani yake katika kuimarisha msikiti, kuswali mkusanyiko, kukusanyika watu kwa imamu wao na kusalimika kutokamana na msongamano na ugumu.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: 48 mas-alatu fiy Swiyaam, uk. 15
  • Imechapishwa: 11/04/2021