07. Hadiyth ya kwamba kuumikwa kunaharibu swawm ni Swahiyh?


Swali 7: Upi usahihi wa Hadiyth:

“Amefungua mwenye kufanya chuku na mwenye kufanyiwa.”?

Jibu: Hadiyth hii ameisahihisha Imaam Ahmad (Rahimahu Allaah), Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah, Ibn-ul-Qayyim na wahakiki wengine. Ni Swahiyh. Ni yenye yenye kuendana kwa njia ya kinadharia. Kwa sababu anayefanyiwa chuku anatokwa na damu nyingi zinazoudhoofisha mwili. Mwili unapodhoofika anahitajia chakula. Kwa hivyo mfungaji akihitaji kufanya chuku na akafanyiwa, basi tunamwambia afungue kwa kula na kunywa ili arudishe nguvu kwenye mwili. Akiwa si mwenye kuhitaji kufanya hivo basi tunamwambia asiumikwe ikiwa ni funga ya lazima kwa ajili ya kulinda nguvu zake mpaka pale atapofungua.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: 48 mas-alatu fiy Swiyaam, uk. 14
  • Imechapishwa: 11/04/2021